Swali: Ukaufu ni nini na Koga ni nini kama tunavyosoma katika Kumbukumbu 28:22?
Jibu: Turejee.
Kumbukumbu 28:22 “Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa UKAUFU, na kwa KOGA; navyo vitakufukuza hata uangamie”
“Ukaufu” ni ugonjwa wa mazao unaotokana na utandu (fangasi), tazama picha juu. Ugonjwa huu unaposhambulia zao la nafaka basi linapata mabaka mabaka na kisha kunyauka na mwishowe kutozalisha chochote.
Sasa hapo Bwana alikuwa anasema na watu wake Israeli (ambao ni sisi pia) kwamba tutakapomwacha Bwana na kufuata miungu mingine na kuiabudu basi tutakuwa tumefungua milango ya laana juu ya maisha yetu, kwani tutapigwa kwa magonjwa ya mwilini lakini pia mazao ya mashamba yetu yatapiwa kwa magonjwa.. na pia tutapigwa kwa misiba na majanga ya nchi.
Mfano wa magonjwa ya mwilini ni hayo yaliyotajwa hapo (Kifua kikuu, homa na kuwashwa).. na mfano wa magonjwa yatakayoshambulia mimea yetu hata tusipate chakula ni hayo yaliyotajwa hapo (Koga na UKAUFU),
Koga ni utandu mweupe unaoshambulia mimea ambao nao pia ukikamata zao la chakula, basi zao lile linadhoofika na hatimaye kufa. (Tazama picha chini).
Lakini pia mfano wa majanga nchi yatakayotupata ikiwa tutamwacha Bwana ni hayo yaliyotajwa hapo juu (hari ya moto na upanga)..Hari ya moto inayozungumziwa hapo ni vipindi vya ukame na jua kali na upanga unaozungumziwa hapo ni vita (au umwagaji damu).
Na sio kwa mambo hayo tu, bali pia kwa mambo mengine mengi yaliyotajwa hapo katika Kumbukumbu 28 na yasiyotajwa… yote yatatupata ikiwa tutamwacha BWANA MUNGU WETU, na kujitumainisha katika mambo mabaya…
Kumbukumbu 28:58 “Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, Bwana, MUNGU WAKO;
59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.
60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.
Lakini kinyume chake, ikiwa tutamtii Bwana MUNGU WETU, na kwenda katika njia zake, basi tutafanikiwa sana kufungua milango ya Baraka nyingi, wala hatutapatwa na hayo yote (Saswasawa na Kumbukumbu 28:1-14)
Bwana atusaidie na kutuneemesha.
Maran atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.
Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
ATAANGAMIZWA NA KUTENGWA NA WATU WAKE.
About the author