Kututa ni nini? (Mhubiri 2:26).

Kututa ni nini? (Mhubiri 2:26).

Swali: Neno “Kututa” lina maana gani kama tusomavyo katika Mhubiri 2:26?


Jibu: Turejee..

Mhubiri 2:26 “Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na KUTUTA, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.

“Kututa” maana yake ni “KULIMBIKIZA”..

Kwahiyo maneno hayo tunaweza kuyaweka katika Kiswahili hiki.. “Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na KULIMBIKIZA, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo”.

Andiko hili linatufundisha hatari ya kukusanya mali na kulimbikiza, ikiwa tupo nje ya KRISTO. Kwa maana hapo maandiko yanasema, mali za mtu huyo (mkosaji), alizojikusanyia na kujilimbikizia, atanyang’anywa na kupewa yule Mungu aliyemridhia.

Lakini pia mstari huo unatuonyesha thawabu kuu ambazo Mungu humpa yule aliyemridhia. Na hizo si nyingine Zaidi ya HEKIMA, MAARIFA na FURAHA.

Kabla ya kumpa mtu Mali humpa Hekima, Maarifa na Furaha na hivi vitatu ndivyo vitu vya kuvitafuta kwa MUNGU kabla ya kuomba vitu vingine kama Mali. Kama Sulemani aliomba Hekima kwanza na Mungu akampa Hekima na Mali ikawa ni nyongeza.

Hali kadhalika na sisi hatuna budi kutafuta hekima, Maarifa, Ufahamu na Furaha kwa bidii kwani tukiyapata hayo basi hayo mengine tutazidishiwa, na hata tusipoyapokea, bado hekima na maarifa vitabaki kuwa utajiri mkuu.

Mithali 3:13 “Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.

16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.

18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye”

Tafuta Hekima, tafuta Maarifa, tafuta Ufahamu, Busara na Furaha..

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Tofauti kati ya Hekima, ufahamu na maarifa, ni ipi?

NI NANI ANAYEUFUNGA MLANGO WA MAARIFA?.

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments