Swali: Je kwanini Bwana YESU aseme Yuda ni shetani, na kwanini amchague shetani kama mwanafunzi wake?
Jibu: Turejee..
Yohana 6:70 “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, NA MMOJA WENU NI SHETANI? 71 Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara”.
Yohana 6:70 “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, NA MMOJA WENU NI SHETANI?
71 Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara”.
Swali hili linafanana na lile la kwanini Bwana YESU amwite Herode “MBWEHA”.
Luka 13:31 “Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. 32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika”.
Luka 13:31 “Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.
32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika”.
Sasa kiuhalisia Herode sio “Mbweha”, wala Yuda siye “shetani”…Isipokuwa watu hao ndani yao wamebeba tabia za “Mbweha” na “shetani”.. Ni sawa na Bwana YESU anavyojulikana kama Mwanakondoo…haimaanishi Bwana YESU ni kondoo (mnyama), La!, isipokuwa ndani yake (katika roho) ipo tabia ifananayo na ya kondoo yaani ya “unyenyekevu”.
Hali kadhalika Yuda si “shetani” bali ndani yake kulikuwa na roho ya shetani ya usaliti na mauaji.
Luka 22:3 “SHETANI AKAMWINGIA YUDA, AITWAYE ISKARIOTE, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao”.
Luka 22:3 “SHETANI AKAMWINGIA YUDA, AITWAYE ISKARIOTE, naye ni mmoja wa wale Thenashara.
4 Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao”.
Hivyo Bwana YESU alikuwa anamaanisha roho iliyokuwemo ndani ya Yuda na si utambulisho wa YUDA, utaona pia kuna wakati alimwambia Petro kuwa ni shetani..
Mathayo 16:22 “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata. 23 Akageuka, akamwambia Petro, NENDA NYUMA YANGU, SHETANI; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu”.
Hapa Bwana hakuwa anaongea na Petro, wala hakuwa anamkemea Petro, bali ile roho iliyokuwa ndani ya Petro (yaani ya ibilisi) ndio aliyokuwa anaikemea.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Bwana YESU hakumchagua shetani, wala Yuda hakuwa shetani bali alikuwa na roho ya shetani ndani yake.
Na hata leo kuna watu ambao ni “mashetani” katika muktadha huo, kwamba ndani yao kuna roho ya shetani.. Hivyo hatuna budi kila siku kujipambanua na kujipima na kujitakasa, ili tusiwe tusionekane kama mashetani.. na utakaso mkuu ni ule Bwana aliowaambia baadae wanafunzi wake, baada ya kumkemea Petro.
Mathayo 16:23 “Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu. 24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. 25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona”.
Mathayo 16:23 “Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona”.
Hapo baada ya maneno hayo kwa Petro, Bwana anaanza kusema “…Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake..”
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je Yuda alienda wapi, ni mbinguni au jehanamu?
Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?
ZIFAHAMU KAZI KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.
Rudi Nyumbani
Print this post