Nini maana ya “Hefsiba” na “Beula” (Isaya 62:4)?

Nini maana ya “Hefsiba” na “Beula” (Isaya 62:4)?

Jibu: Tuirejee.

Isaya 62:4 “ Hutaitwa tena ALIYEACHWA, wala nchi yako haitaitwa tena, UKIWA; bali utaitwa HEFSIBA; na nchi yako BEULA; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; 

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani”

Hii ni habari ya tumaini la kuinuliwa tena kwa Yerusalemu na Israeli kwa ujumla, Kwamba siku ile watakapomrudia Bwana kwa mioyo yao yote basi nchi yao hiyo Bwana aliyoikataa na kuiacha na kuifanya UKIWA, basi ataibarikia tena na kuifanya kuwa FURAHA yake na ILIYOOLEWA.

Sasa tafsiri ya Hefsiba na Beula tayari imeshatolewa pale..  Hefsiba/Hefziba maana yake ni “Furaha yangu iko kwake” na Beula maana yake ni “Aliyeolewa”.. Haya ni maneno ya kiebrania yenye tafsiri hiyo. Hali kadhalika tafsiri ya “Aliyeachwa” kiebrania ni “Abuba” na “Ukiwa” ni “Shemama”..

Kwahiyo kinyume cha aliyeachwa (Abuba) ni Hefsiba (furaha yangu iko kwake)…. Na kinyume cha shemama(ukiwa) ni aliyeolewa(Beula). Ni majina ya kiebrania yaliyotumika kwa jinsia ya kike (soma 2Wafalme 21:1)

Sasa swali kwanini Mungu atumie lugha hizo za “ndoa” kuzungumza na watu wake?.

Ni kwasababu watu wa Mungu wote kiroho wanafananishwa na “mwanamke aliyeolewa/bibi arusi”

Isaya 54:4 “Usiogope; maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maana hutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujane wako hutayakumbuka tena.

5 KWA SABABU MUUMBA WAKO NI MUME WAKO; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote. 

6 Maana Bwana amekuita KAMA MKE ALIYEACHWA na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako. 

7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya”.

Soma pia Yeremia 31:31-32, 2Wakorintho 11:2 na Ufunuo 21:9 utazidi kuliona jambo hilo..

Kwahiyo ujumbe huo haukuwa kwa Israeli peke yao, bali pia unatuhusu sisi, kwamba tumrudiapo Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, basi tunazo ahadi za Baraka na mafanikio, na majina yetu kiroho yatabadilika na kuwa Hefsiba na Beula…Na furaha ya Bwana itakuwa juu yetu nasi tutakuwa na muunganiko wa kiroho na Bwana YESU.

Isaya 62:1 “Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo. 

2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana.

3 Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. 

4 Hutaitwa tena ALIYEACHWA, wala nchi yako haitaitwa tena, UKIWA; bali utaitwa HEFSIBA; na nchi yako BEULA; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. 

5 Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. 

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; 

7 wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

HAPAKUWA NA NAFASI YA KUPITA KWA YULE MNYAMA ALIYEKUWA CHINI YANGU.

Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments