USIKOSE MAZIKO (Mhubiri 6:3)

USIKOSE MAZIKO (Mhubiri 6:3)

SWALI: Naomba kufahamu nini maaana ya mhubiri 6:3?

Mhubiri 6:3

[3]Mtu akizaa watoto mia, akaishi miaka mingi, nazo siku za maisha yake ni nyingi, lakini nafsi yake haikushiba mema; tena ikiwa, zaidi ya hayo, amekosa maziko; mimi nasema, Heri mimba iliyoharibika kuliko huyo;


JIBU: Mhubiri katika jicho la kibinadamu anaelezea jinsi inavyoonekana kama ni hasara kubwa sana, kwa mtu ambaye amejitaabisha maisha yake yote, kutengeneza heshima, kwanza kwa kuwa na watoto wengi, lakini pia kwa kujinyima raha, kuwekeza vema vitu vyake ili siku za kufa iwe heshima kubwa kwake, hata baada ya hapo aache jina kwa uzao wake wote.

Lakini mambo yanatokea kinyume chake, anakufa kama mtu asiye na kitu, au kwa aibu,  hata baada ya hapo anasahaulika kabisa ijapokuwa aliwekeza muda wake mwingi kujijengea jina.. Sasa mhubiri anasema ni heri mimba iliyoharibika kuliko huyu kwasababu kimsingi mimba huwa inasahaulika kweli muda mfupi,na haiwi na maziko ya watu, lakini haijatabika kwa lolote, kuliko huyu ambaye ametabika sana maisha yake yote, kuacha kumbukumbuku , halafu amesahaulika mfano ule ule wa kama mimba iliyoharibika.

Mfano wa watu kama hawa alikuwa ni Ahabu, ambaye alikuwa na watoto sabini, na ufalme mkubwa lakini alikufa kwa aibu, damu yake ililambwa na mbwa. Pamoja na mkewe Yezebeli ambaye mzoga wake uliliwa kabisa na mbwa, hakuwa na maziko. Ikawa ni fedheha kubwa sana kwao (1Wafalme 22),

Lakini maana hasaa ya huo mstari rohoni ni ipi?

Maziko halisi ni yale ya Mungu. Kukosa maziko ya kibinadamu, hakuwezi kukufanya udharauliwe milele. Lakini ukikosa maziko ya Mungu ni aibu na kudharaliwa milele.

Ukipata fedha zote duniani, ukazaa watoto wengi ambao watalirithi jina lako, ukawa mtu maarufu, mpaka ukawa mfalme wa nchi, jina lako likakumbukwa hata vizazi elfu baadaye, kama hujafa ndani ya Kristo. Ni heri mimba iliyoharibika kuliko wewe. Huna kumbukumbu lolote mbinguni

Mwamini Kristo leo, akuoshe dhambi zako. Jiulize ukifa leo katika dhambi, huko uendako utakuwa mgeni wa nani? Wokovu ni sasa, saa iliyokubaliwa ni leo. Fungua moyo wako mpokee Yesu, hata kufa kwako kuwe kuna thamani.

Zaburi 116:15

[15]Ina thamani machoni pa BWANA Mauti ya wacha Mungu wake.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Maana ya Mhubiri 1:9 “wala jambo jipya hakuna chini ya jua”. 

Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)

Nini maana ya mhubiri 9:11? si wenye mbio washindao katika michezo?

Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments