Maana ya Yohana 20:22 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa;

Maana ya Yohana 20:22 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa;

SWALI: Biblia inaposema ‘Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa’. Je tuna mamlaka ya kufanya hivyo wakati wote?

Yohana 20:22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.


JIBU: Mstari huu ukitafsirika vibaya unaweza kuleta maana isiyosahihi ikidhaniwa kuwa kwa uweza wetu, tunaweza kuwaondolea watu dhambi, na kuwafungia pale tutakapo. Hapana.

Biblia inatuambia mwenye uweza wa kusamehe dhambi kwa namna hiyo ni Bwana Yesu tu.

Luka 5:21 Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? N’nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?

22 Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnahojiana nini mioyoni mwenu? 23 Lililo jepesi ni lipi? Kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, uende? 24 Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.

Lakini kwanini Bwana Yesu atoe mamlaka yake Kwa mitume wake?

Ni kufuatana na ahadi aliyowaahidia ndani yao, ambayo ni Roho Mtakatifu tunayoisoma katika huo mstari wa 22. “Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu”.

Kazi ya Roho Mtakatifu ni kumshuhudia Kristo. Hivyo mitume walipewa ushuhuda wa Kristo ndani yao (ndio Injili). Na kwa kupitia hiyo, mamlaka ya kufunga na kufungua wanakuwa nayo, ndani ya hiyo hiyo injili.

Hivyo walipokwenda kuhubiri, na watu wakaamini. Walipotamka kusamehewa dhambi zao, basi wale watu walisamehewa. Vilevile walipokwenda kuhubiri, kisha injili yao ikapingwa, wakakatishwa tamaa na kuacha kuhubiri hapo, mpaka wakafikia hatua ya kuwakung’utia mavumbi yao, Basi hiyo nyumba au huo mji rohoni umefungiwa dhambi. Hauwezi kuokoka kwa namna nyingine yoyote, mpaka watakapokuwa tayari kugeukia injili ya wale waliopelekwa.

Mathayo 10:13 Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.

14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung’uteni mavumbi ya miguuni mwenu.

15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma na Gomora kustahimili adhabu ya siku ya hukumu, kuliko mji ule.

Hiyo ndio namna ambayo watu wa Mungu, huondoa dhambi na kufungia dhambi wanadamu.

Mamlaka hii pia Yesu ameiweka katika kanisa.

Kwasababu kanisa pia ni mwili wake, Hivyo ikiwa yupo mwamini mmoja ambaye alitenda dhambi, akakutwa na mabaya, basi kanisa linaweza kumwombea, akasamehewa dhambi (Yakobo 5:14).

Lakini pia ikiwa yupo ambaye ni mwasi, ameiacha njia, anapoonywa mara kadhaa kisha harejei kwenye mstari, ndugu anapomwacha au kanisa linapomtenga moja kwa moja, basi Mungu naye anamhesabu kama mtu wa mataifa asiyeamini.(Mathayo 18: 15-18,)

Hivyo ni vema kufahamu, mamlaka hii ipo, kwenye injili ya Kristo, lakini pia ipo ndani ya kanisa. Kila mmoja anapaswa amtii Kristo kupitia watumishi wake. Kwasababu lolote walitendalo si wao bali ni Roho Mtakatifu ndani yao, aliyewavuvia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya andiko hili  “Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.(Yohana 5:37)”

MAOMBI KWA WENYE MAMLAKA.

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments