Kwanini Eliya afunge Mbingu miaka mitatu na nusu? (1Wafalme 17:1)

Kwanini Eliya afunge Mbingu miaka mitatu na nusu? (1Wafalme 17:1)

Swali: Ni ipi sababu ya Nabii Eliya kufunga mbingu, mvua isinyeshe kwa miaka mitatu na nusu?


Jibu: Turejee..

1Wafalme 17:1 “Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu”.

Sababu kuu ya Mungu kufunga Mbingu kwa muda wa miaka mitatu na nusu kupitia kinywa cha Eliya nabii, ni MAOVU ya wana wa Israeli pamoja na mfalme wao aliyeitwa Ahabu.

kwani mfalme Ahabu wa Israeli alimwoa YEZEBELI, mwanamke wa nchi ya Lebanoni  aliyekuwa Mchawi na kahaba na mwenye kumwabudu mungu baali (2Wafalme 9:27), na hivyo akawakosesha Israeli wote, na kuwafanya wamwambudu mungu baali badala ya MUNGU WA MBINGU NA NCHI.

Sasa kitendo cha Taifa zima kumwacha Mungu wa Israeli na kwenda kuabudu miungu mingine, ni Kosa kubwa sana na lenye matokeo makubwa sana kwa Taifa..

Sasa kwa kosa hilo la Mfalme, na malkia wake na Watu karibia wote wa Israeli kumwabudu baali, ndio ikapelekea MUNGU kuadhibu nchi nzima kwa kufunga mbingu mpaka mioyo yao ilipofunguka na kumgeukia Bwana.

Na utaona MUNGU alishatangulia kuwatahadharisha wana wa Israeli kupitia kinywa cha Nabii Musa, kuhusiana na makosa ya kuabudu miungu mingine na matokeo yake, KUWA MBINGU ZITAFUNGWA..

Kumbukumbu 11:16 “Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu;

17 hasira za Bwana zikawaka juu yenu, NAYE AKAFUNGA MBINGU KUSIWE NA MVUA, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo Bwana”.

Na utaona pia Maombi ya Mfalme Sulemani, wakati analiweka wakfu lile Hekalu yalilenga hayo hayo…

1Wafalme 8:35 “Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, wakati ule utakapowatesa;

36 basi, usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; unapowafundisha njia iliyo njema, iwapasayo kuiendea; ukanyeshe mvua juu ya nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi wao”.

Hivyo hiyo ndio sababu ya mbingu kufungwa wakati wa Eliya, (maovu ya kumwabudu baali), na ndio maana utaona pale walipojinyenyekeza tu na kutubia, basi Eliya aliomba na mbingu zikafunguka.

1Wafalme 18:38 “Ndipo moto wa Bwana ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji.

39 Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu.

40 Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.

41 Naye Eliya akamwambia Ahabu, Haya! Inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele”.

Na jambo kama hili bado linaendelea kiroho na kimwili, kama tukimtumikia Bwana basi Bwana atatunyeshea mvua yake ya Baraka, lakini kama tutamwacha basi mbingu za Baraka zitafungwa, hivyo huu si wakati wa kusita sita katika mawazo mawili, bali ni wakati wa kufanya maamuzi thabiti ya kusimama na Bwana.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Baali alikuwa nani?

YEZEBELI ALIKUWA NANI

RUHUSU TOHARA IPITE JUU YA KARAMA YAKO.

Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).

Rahabu kwenye biblia.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments