Kwanini Mungu azungumze na Ayubu kupitia upepo wa kisulisuli (Ayubu 38:1)

Kwanini Mungu azungumze na Ayubu kupitia upepo wa kisulisuli (Ayubu 38:1)

Ayubu 38:1

[1]Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,


JIBU: Tukumbuke kuwa Mungu ana njia nyingi za kuzungumza na watu. Na kila njia huwa na maana fulani nyuma yake.

Utakumbuka Alipokutana na Musa alizungumza naye katika kijiti kinachoungua lakini hakiteketei..Kuwafundisha wana wa Israeli kuwa atakuwa pamoja nao hata katika moto wa majaribu lakini hawatateketea kabisa.. 

Kwamfano akina Shedraki, Meshaki na Abednego, walipojaribiwa kwa kutupwa tanuruni, hawakuungua au Danieli kwenye tundu la simba, hakupatwa na dhara lolote kwasababu walimtumaini Mungu. 

Kutufundisha kuwa hata  sasa, na sisi tuliomwamini Kristo, hakuna jaribu la aina yoyote linaloweza kutufanya sisi tuangamie na kupotea mbali na uso wa Mungu. Kwasababu yeye yupo nasi sikuzote.

Halikadhalika tunaona na hapa pia anamtokea Ayubu katika upepo wa kisulisuli..

Kisulisuli hutafsirika kama aina nyingine ya janga, mfano tu wa gharika au tetemeko. Kazi ya kisulisuli huwa ni kuzomba vitu  dhaifu labda makapi, au vitu ambavyo havina msingi imara…

Isaya 40:24

[24]Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu. 

Hivyo Mungu kutumia njia hii, ni kumwonyesha Ayubu kwamba hata katika zomba-zomba za kiroho yeye yupo huko na watu wake.

Vitu vyote vya Ayubu vilizombwa, Kuanzia mali, watoto,.mifugo, hadi mke wake kwasababu ya udhaifu wa imani akazombwa na hila za shetani. Wao wakidhani kuwa Mungu amewaacha kumbe alikuwa nao daima. Tufahamu kuwa dhoruba, tufani, giza, au mwanga..vyote kwake ni sawasawa.

Lakini pia kuna wakati Mungu anazungumza katika utulivu. Utakumbuka tena habari ya Eliya wakati ule anamfuata Mungu kule mlima Horebu, akitarajia Mungu aseme naye katika fujo. Lakini hakumwona Mungu, katika matetemeko wala moto, bali katika sauti ndogo ya utulivu.

Kuonyesha kuwa Mungu husema nasi pia katika utulivu.

1 Wafalme 19:11-12

[11]Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za BWANA. Na tazama, BWANA akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za BWANA; lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 

[12]na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. 

Hivyo ikiwa umeokoka na umesimama imara na Bwana ni vizuri kufahamu kuwa nyakati zote, Mungu yupo nasi. Ni kawaida watu wakishapitia changamoto fulani hufikiri kuwa Mungu hayupo nao, kumbe sivyo nyakati zote nm ziwe za majaribu, za visulisuli, za mafuriko n.k. Tunapaswa tumwone yeye,.kwasababu yupo pamoja na sisi.

Kwasababu ndiye msaada wetu.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JINSI YA KUSHINDA VISULISULI(Mithali 10:25)

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments