Je Bwana YESU alipanda mlimani na wanafunzi wake baada ya siku sita au nane?

Je Bwana YESU alipanda mlimani na wanafunzi wake baada ya siku sita au nane?

Swali: Je Bwana YESU alipanda mlimani na wanafunzi wake baada ya siku ngapi?..ni Sita au Nane?, Kwa maana katika Mathayo 17:1 na Marko 9:2 panaonyesha ni baada ya siku sita (6) lakini tukisoma Luka 9:28 panaonyesha ni siku ni nane (8) Je ukweli ni upi?.


Jibu: Turejee mistari hiyo..

Mathayo 17:1 “Na baada ya SIKU SITA Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani”

Hapa ni kweli tunasoma “Siku sita” na Marko 9:2 tunasoma vile vile ni siku sita (6).

Tusome tena Luka 9:28..

Luka 9:28  “Baada ya maneno hayo yapata SIKU NANE, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba”.

Hapa tunasoma ni siku nane (8) na si sita tena, swali ni je! Biblia inajichanganya?, au mwandishi mmoja amekosea?

Jibu ni La! Biblia haijichanganyi na wala hakuna mwandishi aliyekosea, wote wapo sawa na maneno yote ni hakika, kwasababu biblia ni kitabu kilichohakikiwa na Roho Mtakatifu mwenyewe na hakina makossa (Mithali 30:5).

Sasa kama ni hivyo kwanini  panaonekana  kuna tofauti ya siku?..

Mwandishi wa kitabu cha Luka alionyesha jumla ya siku walizokaa mlimani, na Mwandishi wa kitabu cha Mathayo na Marko wakaonyesha siku walizoondoka katika makazi yao na kuelekea mlimani.

Sasa ni kwamba baada ya Bwana kuwaambia wanafunzi wake kuwa wapo ambao hawataonja mauti hata watakapoona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu, zilipita siku sita akawachukua wanafunzi wake baadhi (ambao ni Petro, Yohana na Yakobo) akapanda nao mlimani.

Na biblia haijaeleza katika hizo siku sita kabla ya kupanda mlimani walikuwa wanafanya nini au walikuwa wapi, pengine waliachana kidogo, au walikuwa katika huduma zilizowatenga kwa muda siku sita, mpaka ilipofika siku hiyo ya kupanda mlimani….hiyo yote haijaeleza lakini inasema tu baada ya siku sita alipanda nao mlimani, na ndicho Mwandishi Mathayo na Marko walichokieleza.

Lakini sasa Luka yeye hakulenga kuelezea siku waliyopanda mlimani, kwamba ni baada ya siku sita za yale maneno, bali yeye alisema “YAPATA SIKU NANE”… Hilo Neno “Yapata” ni neno la ujumla, likielezea Muda wa safari Nzima, kuwa ni SIKU NANE (8), Maana yake baada ya siku sita walipanda mlimani sawasawa na Mwandishi Mathayo na Marko na kule mlimani walikaa siku mbili (2), na kufanya jumla ya siku kuwa nane, ndicho mwandishi alichokilenga. (kwahiyo muda waliokaa mlimani ni siku mbili, lakini walipanda baada ya siku sita).

Kwahiyo biblia haijajichanganya hapo, bali ni uelewa wetu ndio unaojichanganya.

Je umempokea BWANA YESU?.. Na je unajua kuwa dalili zote zinaonyesha kuwa kizazi tulichopo ni cha mwisho?..Je umejiandaaje? Taa yako inawaka?

Luka 12:35  “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;

36  nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na

Je bado unaendelea na maisha ya dhambi?, bado unakunywa pombe?, bado unazini, bado unajichua, bado unavaa kidunia?

Muda umeisha, msikilize Roho Mtakatifu, na usizisikilize roho zidanganyazo.

1Timotheo 4:1“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”

Maran tha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

TABIA SITA (6) ZA WANAFUNZI WA YESU.

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

Je maombi ya mlimani yana ulazima wowote kwa mkristo?

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments