Zifuatazo ni baadhi ya tabia za kuigwa walizokuwa nazo wanafunzi wa Bwana YESU ambazo nasi tunapaswa tuzionyeshe.
1. WALIJIKANA NAFSI ZAO.
Hii ni sifa ya kwanza waliyokuwa nayo wanafunzi wa YESU, Kwani mtu aliyekosa hii sifa hakuweza kuwa mwanafunzi wake.
Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.
Halikadhalika na sisi kama wanafunzi wa Bwana ni sharti tujikane nafsi kila siku, na kubeba msalaba. (Zingatia hilo neno, “Kila siku”), na si siku moja tu..
Luka 9:23 “Akawaambia wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate”.
2. WALIKAA KUFUNDISHWA NA BWANA.
Maana ya kuwa mwanafunzi ni kuketi na kufundishwa mpaka kuhitimu. Na wanafunzi wa Bwana YESU walilijua hilo, hivyo walikuwa walijiunga na chuo hicho cha Bwana ili kupokea mafunzo.
Na leo ni hivyo hivyo, Mwalimu wetu ni ROHO MTAKATIFU na chuo chetu ni Biblia. Na kila mtu ni lazima apite chini ya chuo hicho, ili aweze kuwa mwanafunzi wa Bwana.
3. WALIMFUATA BWANA KILA ALIKOKWENDA.
Maisha ya Bwana YESU hayakuhusisha kukaa mahali pamoja, bali kuzunguka huku na kule, katika miji na vijiji kuhubiri injili.
Mathayo 9:35 “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina”.
Hata wanafunzi wasomao chuo, upo wakati wanaenda katika mafunzo kwa njia ya vitendo kabla ya kuhitimu (maarufu kama mafunzo ya field).
Na vivyo hivyo na sisi kama wanafunzi ni lazima tuifanye kazi ya Bwana kwa yale tuliyoyapokea hata kama hatubobea katika hayo..
Lakini utaona leo, mtu hataki kuwahubiria wengine kwa hofu ya kwamba yeye hajui….Ni kweli usifundishe usichokijua lakini kile kidogo ambacho umeshakijua, usikifukie chini bali kawape wengine wasiokijua kabisa.
4. WALIMTII BWANA.
Tabia nyingine ya mwanafunzi Halisi ni UTII na NIDHAMU.
Wanafunzi wa Bwana YESU wale 11 walimtii Bwana kwakila jambo, kuanzia maagizo ya ubatizo, kuhubiri, meza ya Bwana na mengineyo.
Na wote walimwogopa Bwana (hakuna aliyedhubutu kuhojiana naye wala kushindana naye) Luka 9:45.
5. WALIMWAMINI BWANA.
Wanafunzi halisi wa Bwana YESU hawakuwa na mashaka mashaka na Bwana YESU…walimwamini moja kwa moja…
Yohana 2:11 “Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini”
6. WALIMVUMILIA BWANA
Hata kama yalikuwepo mambo ambayo yalikuwa ni magumu kueleweka kwa katika hali yao.ya uchanga…lakini walivumilia wakiamini siku moja watakuja kuelewa vizuri..
Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? 68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.”
Yohana 6:67 “Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka?
68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.”
Na sisi kama wanafunzi wa YESU hatupaswi kurudi nyuma, tunapokutana na mambo tusiyoyaelewa katika imani au maandiko..badala yake tunapaswa kuwa wavumilivu kwa matumaini mazuri yajayo.
Na kumbuka maana ya kuwa MRISTO ni kuwa MWANAFUNZI…Huwezi kusema ni mkristo na sio mwanafunzi.
Matendo ya Mitume 11:26 “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo ANTIOKIA”.
BWANA ATUSAIDIE.
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)
HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.
Rudi Nyumbani
Print this post