JIBU: Safina ya Nuhu ilikuwa ni mfano wa Meli kubwa iliyojengwa katika deka tatu, ambayo vipimo vyake vilikuwa ni mikono mia tatu urefu wake, na mikono hamsini upana, na mikono thelathini kwenda juu.
Mwanzo 6:13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami. 15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; mikono mia tatu urefu wa safina, mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake.
Ambayo kwa vipimo vya sasa ni sawa na makadirio ya;
> Mita 137 urefu
> Mita 23 upanda
> Mita 14 kimo.
Ukubwa wa ile Safina, kwa sasa tunaweza kuifananisha na hizi meli kubwa za mizigo.
Yapo mambo manne ya kufahamu;
1). Jambo la kwanza ni kuwa hawakuingizwa wengi wengi, bali wawili wawili, na wengine saba saba, hivyo ni idadi ndogo tu ya kila jamii ndio iliyoingizwa.
2) Lakini pia kuna uwezekano Nuhu aliwaingiza wale wadogo wadogo tu, na sio wale wakubwa, Hivyo ikaachilia nafasi ya wanyama wote kujitosheleza ndani ya safina.
3) Tatu alipoambiwa awaingize wanyama kwa “namna” zao, (Mwanzo 6:20). Kwa lugha ya kibiblia si lazima imaanishe kila familia za wanyama ziingie, mfano familia mbalimbali za mbwa, wenye manyoya marefu, wenye asili ya ufupi, wawindaji, n.k. hapana, bali walipoingizwa mbwa, ni namna moja tu, iliwakilisha wote, Na baadaye walipoongozeka waliweza kuonekana wa maumbile tofauti tofauti tena, hilo linawezekana, ni sawa na sisi wanadamu tulitoka katika asili ya baba mmoja na mama mmoja, lakini leo hii kuna waafrika, wazungu, wachina, waarabu n.k. Hivyo ikiwa aliwaingiza kwa njia hiyo basi kisayansi inawezekana kabisa.
4) Lakini hoja ya mwisho iliyo na nguvu kuliko zote, ni kuwa hata kama ni namna zote na familia zao waliingia, bado Mungu anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyafanya, ikiwa katika uzazi wa mwanaume mmoja Mungu amehifadhi mamilioni ya mbegu za kibinadamu, na ndani ya tumbo la mwanamke mmoja hadi watoto tisa wanakaa kwa ujauzito mmoja. Hivyo hatuwezi kushangaa, Mungu kuvihifadhi viumbe vyote katika meli ile, inayoonekana haijitoshelezi. Kwasababu yeye ni Mungu asiyeshindwa na chochote.
Ni kwa yeye haathiriwi na nafasi ya udogo au ukubwa, kusudi lake litasimama tu. Kwa vile vichache vilivyokuwa kwenye safina, ulimwengu leo umejawa na viumbe vingi na watu wengi. Wengine wanasema mimi nabanwa na muda hivyo siwezi kumtumikia Mungu, mimi nabanwa na masomo hivyo siwezi kufanya kitu kwa Mungu, mimi nimefungwa gerezani, siwezi kulitimiza kusudi lolote la Mungu. Ndugu Neno la Mungu halifungwi.
Ndugu Paulo alifungwa gerezani akazuiwa kwenda kuhubiri injili katika mataifa kama ilivyo desturi yake, lakini akiwa gerezani aliandika nyaraka ambazo mpaka leo hii zinaendelea kuhubiri injili, zaidi hata ya ziara zake.
Amini uweza wote wa Mungu mahali popote ulipo, bila kuathiriwa na mazingira.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
SAFINA NI NINI?
Mvinje ni mti gani? (Mwanzo 6:14)
About the author