NI KWA NAMNA GANI KRISTO ALIZIBEBA DHAMBI ZETU?

NI KWA NAMNA GANI KRISTO ALIZIBEBA DHAMBI ZETU?

Ili kuelewa Msamaha wa dhambi jinsi unavyofanya kazi, kwamba ni kwa namna gani Bwana YESU alibeba dhambi zetu, twaweza kuelewa kwa kutafakari mfano huu mrahisi.

Katika sheria za Mahakama inapotokea mfungwa aliyehukumiwa  kifungo, akafariki katikati ya kifungo hiko, na ikathibitishwa na jeshi la magereza pamoja na ripoti za madaktari, na akazikwa basi kile kifungo chake kinakuwa kimefika mwisho, na kesi yake inakuwa haiendelei tena (inafutwa)..

Sasa ikitokea yule mtu akafufuka baada ya siku kadhaa anakuwa hana kesi tena (yupo huru) kwani  kesi yake ilishafutwa, kutokana na ripoti za mahakama na madaktari..

Na zaidi sana mahakama haziamini ufufuo, hivyo itaendelea kuamini kuwa yule mtu alishakufa na taarifa zilithibtishwa na jeshi la magereza pamoja na madaktari.

Sasa ni hivyo hivyo kwa Bwana YESU, yeye alikubali kubeba hatia zetu na makosa yetu yaliyo mengi na akakubali kuhukumiwa kama yeye ndiye aliyeyatenda yale makosa..

Lakini alipokuwa anaanza kukitumikia kile kifungo kwa mateso makali (ambayo kiuhalisia yamgekuwa ya daima)..alikufa katikati..

Na sheria ya hukumu ni kwamba kifo kinahitimisha kifungo cha Mtu, hivyo Kristo alipokufa kifungo chake cha adhabu na mateso kikafikia mwisho, akawa hana hatia tena wala ule mzigo wa dhambi (yupo huru na dhambi sawasawa na maandiko).

Warumi 6:7 “kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi”

Lakini muujiza ni kwamba baada ya siku tatu akaonekana yu hai, na kwasababu hukumu yake ilishafutwa kwa kifo chake, akawa huru na kifungo hiko baada ya kufufuka, ndio maana hatuoni akilia kwa uchungu wa maumivu baadaa kufufuka, bali tunaona ana utukufu mwingi.

Kwahiyo laiti Kristo asingekufa angeendelea kuhesabika laana na mwenye hatia kwaajili ya dhambi zetu nyingi alizozobeba, ingempasa aendelee kukaa katika hali ya adhabu daima, na aendelee kutengwa na MUNGU daima.

Wagalatia 3:13 “Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti”

Lakini kifo chake kimehitimisha hukumu yake, ambayo sisi ndio tungepaswa tuitumikie.

Sasa tunapomwamini ndipo tunaingia katika huo mkondo wa kuondolewa dhambi..

Lakini tunapomkataa basi dhambi zetu zinabaki palepale..ni rahisi tu hivyo!.

Je umemwamini Bwana YESU?..Je umebatizwa kwa ubatizo sahihi wa Maji mengi na wa Roho Mtakatifu?.

Kama bado unasubiri nini?…je bado huoni tu gharama kubwa Bwana YESU aliyoingia kwaajili yetu ili tupate ondoleo la dhambi?.

Mpokee YESU leo wala usingoje kesho.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments