Ahadi ya Roho Mtakatifu ni ya kila mwamini. (Matendo 2:39). Ni msaidizi ambaye Mungu alitupa ili kutuwezesha kuishi maisha ya wokovu kwa viwango vya ki-Mungu hapa duniani.
Hivyo siku ile ulipomkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yako. Tayari ulipokea Roho Mtakatifu siku hiyo hiyo.
Isipokuwa Huwezi ukahisi chochote ndani, bali kwa jinsi unavyoendelea kutii kwa kumfuata Bwana utaziona tu kazi zake ndani yako.
Na hizi ndio kazi zake kuu azifanyazo Roho Mtakatifu anapokaa ndani ya mtu;
Yohana 16:13
[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohana 14:26
[26]Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Warumi 8:26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana
hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
Hivyo humfanya aendelee kuishi maisha ya utakatifu (Yohana 16:8)
Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu
1Wakorintho 12:7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo
Roho yeye yule;
9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule
mmoja;
10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho;
mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake
kama apendavyo yeye
Matendo 1:8
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi
wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Hivyo faida zote hizi hudhihirika ndani ya mtu kwa wingi , hutegemea jinsi mtu huyo anavyompa Roho Mtakatifu nafasi ndani yake. Ndio maana ni vema wewe kama mwamini mpya ujue mambo haya ili usije ukajikuta unamzimisha Roho Mtakatifu ndani yako. Ukawa unaisha maisha ya kama mtu ambaye hajaokoka.
Moja ya agizo la Bwana Yesu kwetu sisi, ni kwamba “tujikane nafsi”. Kujikana maana yake ni kuyatakataa matakwa yetu wenyewe ya mwilini na kukubali yale ya Mungu tu. Ulikuwa mlevi unakuwa tayari kukaa mbali na ulevi, ulikuwa ni kahaba unauaga ukahaba wako. n.k.
Kuwekewa mikono kunanyanyua mafuta Ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu kwa namna nyingine. Na matokeo yake ni kuwa unaambukizwa pia neema.. Katika maandiko tunaona wapo watu kadha wa kadha waliojazwa Roho kwa namna hii. (Matendo 8:17, Matendo 19:6 , 2 Timotheo 1:6 )
Kiwango cha chini ambacho Bwana alituagiza ni SAA moja. Zaidi Pia katika maombi yako mwambie Bwana nijalie kuomba kwa Roho ( kwa kunena kwa lugha) ikiwa bado kipawa hichi hakijakushukia, Ni muhimu pia.
Zingatia: Katika uombaji wako,jifunze kutoa sauti, pia jiachie mbele zake. Huwezi kunena kwa lugha moyoni.. ni lazima kinywa kihusike hivyo Jifunze kuomba huku kinywa chako kikitoa maneno kabisa. Hiyo ni nidhamu nzuri katika hatua za ujazwaji Roho.
Tunajazwa Roho Kwa kuitambua sauti yake inatuagiza nini. Na sauti yake ni biblia. mahali Pekee penye uwepo wote wa Mungu ni kwenye Neno lake.
Hivyo zingatia sana hilo. Mkristo ambaye hasomi NENO, kamwe hatakaa aweze kumsikia wala kumwelewa Roho Mtakatifu.
Ukizingatia hayo basi, utaona uzuri wa Roho Mtakatifu ndani yako.
Mafundisho ya ziada kuhusu Roho Mtakatifu
YEYE ATAWABATIZA KWA ROHO MTAKATIFU NA KWA MOTO.
NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?
JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.
Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?
NAMNA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
About the author