Kanisa kama sehemu ya maisha ya mwamini mpya.

Kanisa kama sehemu ya maisha ya mwamini mpya.

Kama mwamini mpya ni lazima ufahamu kuwa kanisa sio jengo, bali kanisa ni watu wa Mungu waliookolewa na kuwekwa pamoja ili kumwabudu Mungu, na kuhudumiana.

Zifuatazo ni namna mbalimbali ambazo kanisa hutambulika kimaandiko.

i) Kanisa,  hujulikana kama mwili wa Kristo.

1 Wakorintho 12:27

[27]Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.

Kama vile viungo vinavyoshirikiana, vivyo hivyo na wewe huna budi kuwa na ushirika wote wa kanisa, sio kuwa mtembeleaji. Kila mwamini ni kiungo Katika mwili huo.

ii) Hujulikana pia Kama Bibi-arusi wa Kristo.

Waefeso 5:25-27

25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;

Kristo anataka ujue kuwa unapookoka, unakuwa katika kifungo chake, mfano tu wa mwanamke aliye katika ndoa. Bwana mmoja, mwili mmoja, huku akimtii yeye katika yote. Vivyo hivyo na wewe, tangu huu wakati uliokoka ni wajibu wako, kumtumikia Kristo tu, na kumtii katika yote atakayokuagiza ndani ya kanisa.

iii) Kanisa hujulikana pia kama familia ya Mungu. (Waefeso 2:19)

 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu”.

Kama mwanafamilia unakuwa na haki ya kupokea na kurithi ahadi zote ambazo Mungu alizoahidi kwa watu wake, kwasababu wewe  tayari umeshafanywa kuwa mwana wake.

iv) Lakini pia linajulikana  kama hekalu la Mungu

1Wakorintho 3:16 -17

16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.

Kwamba ukishaokoka, wewe na waamini wenzako mnaitwa nyumba ya Mungu, hivyo ni wajibu wako kuifanya nyumba hiyo safi sikuzote kwa  kuishi maisha ya utakatifu, kwasababu Mungu haishi mahali pachafu, bali pasafi. Wewe ni nyumba ya Mungu, iheshimu nyumba yake.

Kwanini kanisa ni muhimu.

  1. Ukuaji Wa kiroho.

Kwa kupitia mafundisho, mahubiri, madara ya uanafunzi, uyapatayo ndani ya kanisa, pamoja na madhihirisho mbalimbali ya  karama za Mungu, utajikuta unajengeka kwa haraka sana na Matokeo yake utajengwa na kukua kiroho, tofauti Na kama ungekuwa peke yako. (Waefeso 4: 11-13)

  1. Kuabudu

Mahali Bora pa kumwabudu, na kumsifu Mungu kwa uhuru na nguvu, ni Pale uwapo katika mkusanyiko. Daudi alisema;

Zaburi 95:6

[6]Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

  1. Maombi na kusaidiana.

Kanisa lina misingi ya maombi na Maombezi. Bwana Yesu alisema;

Yakobo 5:16

[16]Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

Huwezi kusaidika pale unapoishiwa na nguvu, kama huna jamii ya watu nyuma yako kukushika mkono  kimaombi au kihali usimame. Kanisa la kwanza, lilipokusanyika, lilisaidiana katika mahitaji, lakini pia lilitatua migogoro, mbalimbali iliyozuka katikati yao. Hivyo mtu anayekosa kanisa, ukweli ni kwamba anaishi kama yatima wa kiroho.

  1. Kuandaliwa Kwa huduma.

Kanisa Ni kama karakana ya Mungu inayowaandaa watu, kuwa watendakazi. Ni mahali ambapo utatambua Karama yako. Kisha kuitumia hiyo kuwahudumia wengine na kuipeleka mbele kazi ya Mungu.

Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali

Je mahudhurio  ya kikanisa yanapaswa yawe mara ngapi?

Mengi kwa jinsi uwezavyo..

Biblia inatuambia tuonyana kila inapoitwa leo (yaani kila siku).

Waebrania 3:13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;

Pamoja na hilo, atakatifu wa zamani, ukiachilia mbali makusanyiko ya katikati ya wiki, ilikuwa ni lazima siku ya kwanza ya juma wote wakusanyike. (1Wakorintho 16:2). Yaani kila jumapili ilikuwa ni siku ya Bwana.

Ni nini kinatokea pale unapojitenga na kanisa?

  1. Unakuwa dhaifu kiroho, Na mwepesi wa kushindwa na majaribu.
  2. Unakosa Washauri na maongozo ya kiroho.
  3. Karama yako haiwezi kukua na kudhihirika, kwasababu karama hasaa ziliandaliwa kwa ajili ya kanisa.

Kanisa ni kama Shule kwa mwanafunzi. Tunajua Shule kama Shule sio elimu. Bali shule hutoa elimu. Kwasababu ndani yake wapo waalimu, zipo nidhamu, wapo wanafunzi wenzako , yapo majaribio, Vipo vitabu n.k. ambavyo vinakusaidia Kufaulu vizuri katika masomo yako.

Halikadhalika wewe kama mwamini mpya, ni lazima uwe na kanisa. Mwamvuli wako, ujengwe ukue, uandaliwe. Kanisa ni chombo maalumu alichokiunda Mungu, siku ile ya pentekoste ili watu wake wamwone yeye.

Zingatia sio kila mkusanyiko unaosema ni wa-kikisto ni kweli ni kanisa la Mungu. Kwasababu manabii, na wapinga-Kristo wapo sasa duniani.

Hii ni aina ya mikusanyiko ambayo unapaswa ujiepushe nayo;

> Epuka mikusanyiko isiyo mfanya YESU KRISTO kama ndio msingi, na wokovu wa mahali hapo.

> Epuka mikusanyiko isiyokurejeza katika maisha haki na utakatifu.

> Epuka mikusanyiko isiyokukumbusha juu ya hatma ya maisha yajayo, yaani kuzimu na mbinguni

> Epuka mikusanyiko isiyoamini katika utendaji kazi wa karama za Roho Mtakatifu.

Omba, kwanza, kisha fanya maamuzi.

Ikiwa bado hujawa na uhakika wa pa kukusanyika. Basi wasiliana na sisi tukusaidie mahali sahihi pa kukusanyika..

Vifungu hivi visitoke akilini mwako:

Waebrania 10:25

[25]wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

Mhubiri 4:9-10

[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;  Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

[10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

Zaburi 122:1

[1]Nalifurahi waliponiambia,  Na twende nyumbani kwa BWANA.

Haya ni mafundisho ya ziada yatakayokupa mwangaza  juu ya kanisa na taratibu zake.

Kwanini tunakwenda kanisani?

WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA

WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU

EPUKA KUCHELEWA IBADA.

KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.

KAMA MKRISTO NI LAZIMA UWE NA DESTURI HII.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments