Jina la YESU KRISTO lenye nguvu libarikiwe.
Neno la MUNGU linatufundisha kuwa sote tuliomwamini YESU, tumefanywa kuwa “Wahudumu wa Agano jipya”, maana yake tu watumishi na wahudumu wa Agano jipya, ambalo ni Agano la Roho na sio la mwilini.
Na siri kubwa ni kwamba utumishi huu tuliopewa, “Umejitosheleza” asilimia zote, hauna kasoro, ni wenye nguvu wa kubadilisha visivyobadilika, na ni wenye thawabu kubwa kuliko kazi zote.
2Wakorintho 3:6 “Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha”.
Sasa kufahamu kwa undani nini maana ya “Andiko huua bali roho huhuisha” fungua hapa>>> Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)
Lakini ninachotaka tuone siku ya leo ni “Utoshelevu huu tuliopewa” kwamba tunapokuwa wahudumu wa Agano hili jipya tumepata bahati kubwa sana, kwasababu umejaa utoshelevu usio elezeka, na hiyo ndio maana wote wanaomtumikia MUNGU ijapokuwa watapitia dhiki, au mateso, au adha, lakini ndani yao wanajihisi washindi siku zote,
Ndani yao wanajivunia injili, ndani yao wanazo nguvu, hata kama utu wao wa nje unachakaa..
2Wakorintho 4:12 “Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu. …..16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku”.
2Wakorintho 4:12 “Basi hapo mauti hufanya kazi ndani yetu, bali uzima ndani yenu.
…..16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku”.
Kwa ufupi wana heri kubwa wamtumikiao Bwana katika Agano hili jipya kwa mujibu wa Biblia, kwasababu ni wenye thamani na thawabu kubwa mbinguni.
Je wewe ni mhudumu wa Agano jipya?..Je unaitumia karama yako vizuri?.. au umeificha talanta yako ardhini, umepewa huduma ya uinjilisti je unaufanya kwa bidii?.. umepewa karama nyingine yoyote je unaitumia kwa uaminifu?..
Huenda hujui hicho ulichopewa kina uthamani kiasi gani, lakini nataka nikuambie kuwa huduma iliyowekwa ndani yako baada ya wewe kuokoka ni kubwa, na imejitosheleza, kinachotakiwa ni wewe kuanza kazi na sio kuendelea kungoja.
Amka leo kama umelala, anza kuhudumu madhabahuni kwa Bwana, Nenda shambani kwa Bwana kavune watu, thawabu yako itakuwa ni kubwa mbinguni kwani kilichowekwa ndani yako ni kikubwa wala usijidharau au mtu asikudharau, simama mtumikie aliyekuita, kwani muda haukungoji na bado ule mwisho umekaribia sana.
Bwana akubariki na kukuongezea Neema, ikiwa utataka msaada hatua za kuanza katika kumtumikia MUNGU, basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi 0789001312.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
JE UTAKATIFU NI MATENDO YA SHERIA?
UKIMBIE UHURU WA ULIMWENGU
UPENDO WA KRISTO WATUBIDISHA;
Uradhi wa Mapenzi yake ni nini? (Waefeso 1:5)
UFANYE BIDII KATIKA KUSOMA.
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ