YEZEBELI ALIKUWA NANI

YEZEBELI ALIKUWA NANI

Yezebeli, alikuwa ni Binti wa Mfalme wa Wasidoni aliyeitwa Ethbaali (1 Wafalme 16:31). Sidoni ilikuwa ni nchi iliyokuwepo Kaskazini mwa Taifa la Israeli, kwasasa nchi hiyo ni nchi ya LEBANONI.

Desturi za Wasidoni zilikuwa ni kuabudu miungu, waliabudu mungu wao maarufu aliyeitwa BAALI.

Mfalme wa Israeli aliyeitwa Ahabu alimwoa Binti huyo wa kifalme na kumleta katika Taifa la Israeli na kuwa Malkia. Na hivyo kuingiza ibada za miungu migeni ndani ya Taifa la Mungu.

Yezebeli licha tu ya kulichafua Taifa la Israeli kwa kumshawishi sana Mumewe Ahabu, alikuwa pia ni mchawi (2 Wafalme 9:22). Aliwaua manabii wengi wa kweli wa Mungu, na aliikosesha Israeli kwa sehemu kubwa sana. Mahali pengine Inamtaja Yezebeli kuwa ni Nabii wa Uongo. (Ufunuo 2:20)

Yezebeli pia ndio mwanamke pekee kwenye Biblia nzima aliyekuwa anapaka WANJA usoni na kupamba uso. Desturi za wanawake makahaba.(2 Wafalme 9:30). Mwanamke huyu ndiye Mwanamke pekee aliyeshindana na maagizo ya Mungu kuliko wanawake wote kwenye Biblia, ndiye aliyemsumbua sana Eliya na hata kufikia hatua Nabii Eliya kumkimbia, kuogopa madhara atakayoyapata kutoka kwake.

Yezebeli alikuwa na mtoto wa kike, aliyeitwa ATHALIA ambaye naye alirithi tabia zote za mama yake ambaye naye pia alikuwa anaabudu Baali, Athalia alikuwa muuaji na aliutwaa umalkia kwa nguvu ndani ya kabila la YUDA.

Yezebeli hakudumu muda mrefu kwani alikufa sawasawa na unabii uliotolewa juu yake, kwamba atakufa na mbwa watalamba damu yake. Siku ya kufa Yezebeli aliangushwa kutoka juu ya ghorofa refu na kuchuruza damu ukutani mwote, na alipofika chini farasi alimkanyaga kanyaga..na Mbwa walikumla na kubakisha viganja tu vya mikono na kifuvu (2 Wafalme 9:35)

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

NABII ELIYA NI NANI?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments