JIBU: Biblia haituelezi kuwa kama kuna mtu yeyote anayejuwa mawazo ya mtu isipokuwa mtu mwenyewe na Mungu peke yake basi. Mungu peke yake ndio yupo kila mahali, yeye peke yake ndio anajua kila kitu, na yeye peke yake ndiye anayeweza mambo yote..Kwasababu yeye ndio muumba wa vyote. Hilo tunalithibitha katika vifungu hivi vya maandiko.
Zaburi 139: 1 “Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.
2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
4 Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana.
5 Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. 7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu”.
Unaona ni sawa tu! na mtu ambaye anamiliki account ya facebook,sasa mwenye uwezo pekee wa kuiingia na kutoka ni mmiliki wa account hiyo na aliyetoa account hiyo ambao ni facebook basi! Hao wawili tu ndio wenye uwezo wa kufanya lolote juu ya account hiyo lakini mtu mwingine wa nje! hata kama na yeye atakuwa anamiliki shirika kubwa kiasi gani linaloweza kufanana na facebook, hawezi hata kidogo kuwa na uwezo wa kudukua taarifa za account yako ya facebook, labda wewe umfunulie au shirika la facebook lenyewe limpe taarifa zako.
Vivyo hivyo moyo wa mwanadamu shetani hawezi kuuingia wala kufahamu mawazo yaliyopo ndani yake, isipokuwa wewe mwenyewe umfunulie au Mungu.
Lakini pia kumbuka biblia inamwita shetani lile joka la zamani, Hii ikiwa na maana kuwa amekuwepo duniani tangu zamani na hiyo inampa faida kuwatazama wanadamu kwa muda mrefu na kuelewa baadhi ya tabia walizonazo, hivyo anaweza akawa anauwezo wa kuhisi mawazo ya mtu yakoje na haraka akamuundia njia ya kumwangamiza kulingana na anachokitamani, lakini kufahamu moja kwa moja fikra za mtu kama vile Mungu hilo hawezi, uwezo huo wa kuyasoma mawazo ya mtu mwingine hata sisi wanadamu tumepewa,..unaweza ukamuangalia mtu katika mazingira Fulani ukajua anachowaza, lakini huwezi kuingia ndani ya kichwa chake na kujua kila kitu ndani yake.
Na ndio maana utaona shetani alipokuwa anamjaribu hata Yesu alikuwa anamwambia ikiwa wewe ndiwe! Kuonyesha kuwa alikuwa hana hata uhakika wa uhusiano wa Yesu na Baba yake ulivyo maana kama angelijua hilo asingepoteza hata muda wake kumuuliza Bwana maswali yaliyoonekana kuwa ni ya kitoto kwa Bwana .
Lakini pia shetani anaowezo wa kutuma fikra zake ndani ya mtu, anaweza akatuma kwa kupitia ndoto, kwa kutumia mawazo, au hata kwa njia ya maono. Na hayo huwa yanakuja na nguvu Fulani kukushawishi kufanya mambo yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Kama mtu akiwa anaendelea kuyatafakari badala ya kuyakataa basi ndivyo anavyompa shetani wigo mpana wa kuyamiliki maisha yake.
Na ndio maana biblia inasema inatupaswa tuwe na uwezo wa kuteka kila fikra ipate kumtii Kristo. Jambo lolote linalokuja kwenye mawazo yetu, au ndoto, au chochote kile kama kinapingana na kanuni za Mungu ni kutokipa nafasi, kukikataa kwa nguvu, na chenyewe mwisho wa siku kitaondoka.
2 Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;”.
Hivyo, kuhusu shetani kufahamu mawazo ya mtu kana kwamba anasikia radio, hilo jambo haliwezi, japo anao uwezo wa kuhisi mtu au anachokiwaza au kumsoma mawazo yake kwa kuchunguza tabia za huyo mtu na mienendo yake, na mazungumzo yake mara kwa mara.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
TUNAMWABUDU MUNGU ALIYE HAI ,JE! WALE WANAOMWABUDU SHETANI SIO MUNGU WAO ALIYE HAI?
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
About the author