Katika Warumi 8:18-25. Je! Viumbe vinatazamiaje kwa shauku kufunuliwa kwa Mwana wa MUNGU?

Katika Warumi 8:18-25. Je! Viumbe vinatazamiaje kwa shauku kufunuliwa kwa Mwana wa MUNGU?

JIBU: Jambo lisilofahamika na wengi ni kwamba, viumbe navyo vitakuwepo katika ulimwengu ujao (Mbingu Mpya na nchi Mpya)..Mungu alipoiumba dunia hakuwaumba wanadamu peke yao, bali aliwaumba pamoja na wanyama na ndege, Na Mwanadamu alipoasi, laana aliyolaaniwa haikumpata Mwanadamu peke yake bali hata na wanyama, mwanadamu alipoambiwa atakufa, na wanyama pia walikufa, Mwanadamu alipoambiwa atazaa kwa uchungu wanyama nao pia walizaa kwa uchungu.  

Mungu alipoiangamiza dunia kwa gharika, wanyama nao waliangamizwa..na kadhalika Mungu alipowaokoa baadhi ya wanadamu wachache katika safina (Nuhu na wanawe) pia kulikuwepo na baadhi ya wanyama waliookoka na gharika. Hivyo mahali popote mwanadamu alipo wanyama nao wapo, kwasababu waliumbwa kwa ajili ya mwanadamu.   Kwahiyo kama vile sisi wanadamu tunavyotamani siku ya kufunuliwa kwetu, yaani siku tutakayoiingia Mbingu Mpya na Nchi Mpya, siku ambayo hatutakiona tena kifo, wala uchungu, wala shida na wanyama na viumbe vyote vivyo hivyo vinatamani kama sisi. Navyo vinatamani kutoka katika laana hii ya dhambi, na kuingia uhuru wa Umilele.

  Biblia inasema katika ulimwengu ujao ulimwengu utakuwa na Amani, kutakuwa hakuna dhiki kwa wanyama, wala tabu. Wanyama hawatakulana tena, simba atakula majani kama ng’ombe, na mbwa mwitu atakaa pamoja na mwanakondoo.

  Isaya 11: 6 “Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe.

8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.

9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari”.

Kwahiyo wanyama na viumbe vyote vinatamani siku ya kuwekwa kwao huru kufike, kama sisi tunavyotamani siku hiyo ifike.

  Mungu akubariki.


Mada Nyinginezo:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

JE! NI KWELI KUNA VIUMBE VINAVYOISHI SAYARI NYINGINE (ALIENS)?

NUHU ALIWALETAJE WANYAMA WOTE KWENYE SAFINA

MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!

SEHEMU ISIYO NA MAJI.

KISASI NI JUU YA BWANA.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments