Kuna tofauti kati ya kuwaza na kutafakari, kuwaza ni kitendo cha kurudia rudia kwenye akili yako ile kumbukumbu ambayo tayari unayo, kwa mfano labda mtu kutwa nzima alikuwa yupo sokoni anatafata mboga nzuri ya kununua….Sasa wakati yupo katika utulivu ametulia anajikuta akili yake inaanza kufikiria yale mambo ambayo alikuwa anayaona, aina za mboga, nafaka, matunda n.k…yaani mtu huyo akili yake inakuwa inazunguka kwenye kile tu alichokiona..
Lakini kutafakari ni tofauti na kuwaza, Kutafakari sio tu kurudia rudia kwenye akili kile ulichokiona au kukifanya, hapana bali kwenda mbali zaidi ni kitendo cha kutathimini kwa undani vile ulivyoviona..kwamfano tuchukue ule ule mfano wa sokoni, mtu anayetafakari anajiuliza maswali mengine kichwani kwake, Je! Zile mbona zinatolewa wapi? Mbona sizioni zikilimwa mkoani kwetu, atajiuliza lile soko kwanini limewekwa pale, na kwanini aina ile ya nafaka inauzwa na watu wengi zaidi, je! Wanunuzi wa hapa ni watu wa aina gani, Je kazi wanaoifanya hapa inawalipa vizuri? n.k..,Sasa mtu anayewaza kwa namna hiyo, huyo ndiye anayetafakari , na utaona mtu wa namna hiyo mwishowe huwa anakuja na suluhisho lilio bora zaidi, pengine na yeye utamwona siku moja pale sokoni amekuwa muuzaji.
Vivyo hivyo na katika biblia, tunapaswa tulitafakari Neno la Mungu, na sio kuliwaza tu, tunaposoma biblia tunapaswa tujiulize je! Hii hadithi inafunua nini rohoni?, Je! Tafsiri yake katika maisha yetu ni nini, Mungu hapa alikuwa na maana gani kusema hivi, ni kwanini afanye vile, na asifanya hivi,,Sasa mtu unapokuwa katika hali ya maswali na namna hiyo katika kusoma kwako biblia, mawazo yako yanapata kibali mbele za Mungu na ndipo Roho Mtakatifu anachuka nafasi ndani yake kukufundisha na kukumfunulia..
Zaburi 19: 14 “Maneno ya kinywa changu, NA MAWAZO YA MOYO WANGU, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu”.
Tofauti na Yule ambaye anasoma tu hadithi labda tuseme ile ya YONA jinsi alivyomezwa na samaki, anatoka pale anaifurahia ile hadithi anaiwaza tu juu juu jinsi alivyomezwa na samaki Yule na jinsi alivyotapikwa halafu basi ile hadithi inabakia tu kichwani kwake kama kumbukumbuku, hakuna kingine chochote za ziada anaweza kujiuliza juu ya hilo. Mtu kama huyo Neno la Mungu litabakiwa kuwa fumbo kubwa ndani yake, japo anaweza kujiona anaifahamu biblia nzima. .. Lakini kama mtu akiitafakari kwa undani ndipo hapo Roho Mtakatifu anampa ufunuo mkubwa kama ule wa YESU kukaa kaburini siku tatu kwa kupitia tu kuitafakari habari ya Yona.
Halikadhalika Bwana Yesu aliposema yatafakarini maua, watafakarini kunguru..(Luka 12:24) Ni zaidi ya kuwaangalia tu wanavyoruka, bali jinsi wanavyoishi, wanavyokula bila kupanda, bila kuvuna, wasivyojiwekea hazina ghalani, wasivyomeza vidonge n.k. Hivyo tukiweza kutafakari Neno la Mungu kwa namna hiyo Roho Mtakatifu hatapata shida kutufunulia siri zake kiwepesi.
Ni wajibu wetu kulitafakari Neno lake kila siku.
Ubarikiwe sana.
Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba
+225693036618/ +225789001312
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
TABIA YA KIPEKEE USIYOIJUA KUHUSU NENO LA MUNGU.
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
HATARI YA KUTOKUITAFAKARI BIBLIA VIZURI?
About the author