Vifo vya mitume wa Yesu/ jinsi mitume walivyokufa.
Mtume pekee ambaye biblia inarekodi mauaji yake jinsi yalivyokuwa ni mtume Yakobo ndugu yake mtume Yohana. Huyu biblia inasema katika Matendo 12:1-2, kuwa Mfalme Herode alimuua kwa Upanga, alikatwa kichwa. Lakini kwa habari ya mitume wengine waliosalia biblia haijarekodi jambo lolote kuhusu vifo vyao.
Hivyo ili kupata taarifa zihusuzo huduma zao na vifo vyao ilipasa watu warejee katika hadithi ambazo zinaamika ziliandikwa na watu ambao walikuwa karibu sana na mitume, au walioshuhudia vifo vyao. Japo habari hizo hatuwezi kuzithibitisha kuwa zina usahihi wa asilimia mia, lakini kwa sehemu kubwa zimethitishwa kuwa kweli, kulingana na kupatana kwa maneno ya mashuhuda.
Mathayo alijeruhiwa vibaya na upanga alipokuwa anahubiri katika nchi ya Ethiopia kaskazini mwa Afrika. Na baadaye kukumbwa na mauti kutokana na pigo la jeraha hilo..
Wakati wa wimbi kubwa la dhiki za wakristo likishamiri huko Rumi , walimkamata Mtume Yohana na kumzamisha katika karai la mafuta yaliyotokota ili afe, lakini aliokoka kimiujiza. Wakamchukua na kumpeleka katika kisiwa cha Patmo, na huko ndipo alipoandika kitabu cha Ufunuo. Lakini baadaye aliachiwa huru na kurudi Asia ndogo ili kupeleka barua zile kwa yale makanisa saba huko Asia ndogo. Ambayo kwa leo inajulikana kama nchi ya Uturuki. Huyu ndiye mtume pekee aliyekufa kifo cha Amani katika uzee.
Mtume Petro aliuawa huko Rumi, inasemekana, walimkamata na kusulibisha kichwa chini miguu juu, kutimiza unabii Bwana Yesu aliompa katika:
Yohana 21;17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
18 Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka.
19 Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.
Hivyo ndivyo vifo vya mitume wa Yesu vilivyokuwa.
Alikuwa ni mmishionari huko Asia, aliuliwa kwa kuchapwa na mijeli mikali mpaka kufa. Unaweza ukaona jinsi mitume walivyokufa kikatili.
Walimkamata na kumfunga katika msalaba uliolazwa kama alama ya “X”. Kisha wakamwacha akiwa amefungwa kwa muda mrefu ili kumwongezea mateso ya kufa kwake, huko ukigiriki. Na Wale waliokuwa wakimfuata mfutua walisema walimsikia akisema maneno haya;
Nukuu: ”Kwa muda mrefu, nimekuwa nikiingojea kwa hamu saa hii, msalaba umekuwa wakfu sikuzote kwa mwili wa Kristo kutundikwa juu yake”.
Aliendelea kuhubiri injili mbele ya wale watesi wake akiwa pale msalabani kwa siku mbili, mpaka mauti ilipomkuta.
Alipigwa mkuki katika moja ya ziara zake za kuhubiri injili na kupanda makanisa kule India.
Aliuawa kwa kusulibiwa alipokuwa akiitaabikia Injili huko kaskazini mwa Asia ndogo,.Alikamatwa kwanza na kutupwa gerezani, kisha baadaye wakaja kumsulubisha. Mwaka 54 W.W
Aliuawa kwa kusulibiwa mwaka 72 W.W huko Eddessa.
Alihubiri injili Mauritania, na baadaye Uingereza ambapo huko ndipo naye alipokuja kusulibiwa.
Huyu ndiyo yule mtume aliyechukua nafasi ya Yuda aliyemsaliti Yesu. Historia inarekodi alipigwa naye kwa mawe na mwishowe kukatwa kichwa.
Huyu alijinyonga baada ya kupata maumivu makali ya kumsaliti Yesu kwa vile vipande 30 vya fedha.
Paulo ambaye hakuwa miongoni mwa wale mitume 12, Aliteswa na jemedari wa Kirumi Nero, na baadaye akaja kukatwa kichwa.
Mitume wengine kama vile, Luka alitundikwa juu ya mti wa mizeituni kutokana na msimamo wake na Imani yake thabiti kwa Kristo..N.k. wapo mitume wengine pia waliouwa kwa njia mbalimbali wameandikwa katika vitabu vya historia za wakristo ukipenda unaweza kusoma mwenyewe kitabu kinachoitwa FOXES BOOK OF MARTYRS.. Hivyo ndivyo vifo vya mitume wa yesu/ jinsi mitume walivyokufa.
Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu”
Wingu kubwa la mashahidi linatuzunguka mimi na wewe. Watu waliokuwa tayari kufa lakini wasiiache Imani. Kwasababu walikuwa wanajua thawabu iliyowekwa mbele yao ni kubwa kiasi gani. Vilevile walikuwa anajua hukumu itakayowapata kama wakiikana Imani ni kubwa kiasi gani.
Ukiwa bado upo nje ya Kristo, kumbuka kuwa mlango wa neema hautakuwa wazi siku zote. Tubu leo umgeukie muumba wako. Unachotakiwa kufanya Hapo ulipo chukua muda mchache piga magoti. Kisha anza wewe mwenyewe mweleze Mungu makosa yako yote. Na kwamba unahitaji msamaha. unahitaji msaada kutoka kwake kukusaidia kuushinda ulimwengu.
Hivyo Ikiwa utatubu kwa kumaanisha kutoka moyoni mwako. Basi ujue kuwa Mungu yupo hapo kukusikia. Na atakusamehe dhambi zako zote. Na kukuosha kwa damu ya mwanawe YESU KRISTO. Na Amani ya ajabu itaufunika moyo wako kuanzia huo wakati.
Bila kupoteza muda. Nenda katafute kanisa la Kiroho.Ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi. Na kwa jina la Yesu Kristo sawasawa na Matendo 2:38. Na Mungu mwenyewe atakumwagia kipawa chake cha Roho Mtakatifu kukusaidia siku zote. Fanya hivyo sasa na Mungu atakusaidia.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
TUSIPOUTHAMINI WOKOVU TUTAPATAJE KUPONA?
https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/bwana-alimaanisha-nini-aliposema-mtu-akija-kwangu-naye-hamchukii-baba-yake-hawezi-kuwa-mwanafunzi-wangu/
UNYAKUO.
UWE MWAMINIFU HATA KUFA.
UWE MWAMINIFU HATA KUFA.
About the author