KUTOMZUIA MTOTO WAKO NI DHAMBI.

KUTOMZUIA MTOTO WAKO NI DHAMBI.

Shalom, karibu tujifunze biblia…Kuna madhara makubwa sana ya kutombana mwanao..na kumruhusu tu kufanya lolote analojiamulia, kwa kuogopa kuwa atakuchukua…

Mtoto kamwe hawezi kukuchuku! unapomwonya au kumbana.…Hebu jiulize wewe wakati ukiwa mdogo, mzazi wako alipokuzuia au alipokubana ufifanye jambo Fulani je ulimchukia?…ni wazi kuwa hukumchukia zaidi uliona tu ni kama mzazi hakipendi kile kitu na si kwamba hakupendi wewe.

Vivyo hivyo na wewe unapombana mwanao asifanye vitu Fulani Fulani ambavyo unaona vina muelekeo mbaya wa kumletea madhara mwanao huko mbeleni, hufanyi dhambi…unapoona kuna tabia inaanza kukithiri ya kupenda kutazama Tv kwa muda mrefu, usiache kuithibiti hiyo tabia..Unapoona kuna tabia ya kuanza kuzurura zurura…mbane, si kila siku ni ya kwenda kucheza cheza na kutazama Tv, ni lazima ziwepo siku za kujifunza Neno nyumbani, watoto wana vichwa vizuri sana vya kushika mambo/kukariri…Kwahiyo katika hali walizopo ni lazima uwape mistari ya kuishika kichwani, hata kama hawaielewi sasa, lakini itakaa ndani yao kama akiba, watakapokuwa watu wazima itakuwa tayari ipo kichwani, hivyo watakapoanza kuitafakari watakuwa hawana kazi ya pili ya kuikariri tena…

 Na pia ni lazima ziwepo siku za kujisomea masomo ya shuleni wawapo nyumbani, ni lazima yawepo masaa ya kumfundisha mwanao kusaidia vijishuhuli vidogo vidogo..Hata kama hakuna shughuli yoyote ya kusaidia (labda nyumbani wapo wafanya kazi wa kutosha)…usikubali mwanao abweteke, mtengenezee kazi ya kufagia, kupika, kuosha vyombo, kupasi, kufua nguo, kufanya usafi n.k..Pia mtume mahali kama dukani n.k..Na pia unapoona kuna vijitabia vya kiburi na utundu vinaanza basi tumia kiboko kidogo kuvidhibiti…

Mithali 23:13 “Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu”.

sio dhambi na wala hatakuchukia….Usiusikilize uongo wa shetani moyoni mwako kwamba ukimrudi mwanao atakuchukia…Kamwe watoto hawana chuki, wala vinyongo…

Ukiona mtu anakinyongo na mtu Fulani kwa kitu alichofanyiwa utotoni…kiuhalisia kinyongo hicho kilimwingia baada ya yeye kuwa mkubwa na kukitafakari kile kitu kibaya alichofanyiwa…Lakini katika hali ile ya utoto aliyokuwepo hakuwa na ufahamu huo…Hivyo hata mtoto leo hii ukimwadhibu kwa kosa lolote lile hawezi kukuchukia badala yake atajifunza kutokukifanya kile kitu….na siku atakapokuwa mkubwa ndipo atakumbuka zile adhabu na atakapotafakari kwamba ulikuwa unamwadhibu au ulikuwa unambana kwa kwa faida yake mwenyewe ndipo atakapokupenda zaidi…atasema moyoni mwake kama mama/baba asingenizuia na ile tabia yangu sijui leo ningekuwa wapi..na hivyo atakupenda zaidi kuliko kukuchukia lakini tabia ya kutombana mwanao kwa kuogopwa kuchukiwa…nakuambia ukweli siku mtoto Yule atakapokuwa mtu mzima na kutafakari ni jinsi gani ulivyokuwa unamwangalia tu anapotukana, au anapofanya mambo yasiyofaa pasipo kumwambia chochote atakuchukia na kusema hukuwa unamjali.

Kumbuka Uzao wa Tumbo lako ni thawabu yako mwenyewe…Mtoto uliyepewa ukimtunza vyema ni kwa thawabu yako mwenyewe katika siku za baadaye…

Zaburi 127:3 “Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, UZAO WA TUMBO NI THAWABU”.

Mithali 22:6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”.

Pia kama bado hujapata mtoto na umeolewa/umeoa….usiwe na hofu, mwamini Mungu, usijiangalie umri uliopo, hata kama ni miaka 50..wapo waliozaa wakiwa na miaka 90 sembuse wewe mwenye miaka 60?..Kwahiyo wakati wa Mungu ni bora kuliko wa wanadamu..zidi kujitenga na ulimwengu na kuishi maisha ya utakatifu na kumcha Mungu kama kawaida…hayo mengine mwachie Baba, huwa anafanya njia mahali pasipo kuwa na njia, na mahali pasipoonekana dalili….na huwa anarudishaga miaka iliyoliwa na parare kwa watoto wake..Hivyo muamini Mungu na mngojee. Na upatapo mtoto kumbuka siku zote kwamba kutombana kufanya mambo yasiyofaa ni kwa hasara yako mwenyewe na yake pia.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.

USIPUNGUZE MAOMBI.

KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments