“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?

“Shinikizo” ni nini kibiblia, Na maana yake rohoni ni ipi?

Shinikizo ni shimo au kisima fulani kilichotengenezwa mahususi  kwa ajali ya kukamulia zabibu,. Zabibu zinavyokamuliwa leo ni tofauti jinsi zilivyokamuliwa zamani, leo hii ni mashine ndio zinazotumika kukamua juisi. Lakini zamani ilikuwa ni tofauti.

Walichokuwa wanakifanya mara baada ya kutengeneza au kuchimba a kisima hicho, walizitupa zababu ndani yake na kujaa, kisha wanaume walikuwa wanaingia ndani ya kisima hicho na kuanza kuzikanyaga kanyanga, wakisapotiwa na kamba kwa juu, ili wapate uwiano(balance),. Sasa kwa pembeni walikuwa wanatengeneza kimfereji ambacho, kilielekeza juisi yote ya zabibu katika kisima kingine kidogo, ambapo ndani ya hichi kijisima sasa waliweza kuichota juisi ile  ya zababu ikiwa safi kabisa kwa matumizi yao mbalimbali.. Tazama picha juu.

Hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo unaweza kulisoma Neno hilo;

Mathayo 21:33 “Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.

34 Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake”.

Hagai 2:16 “katika wakati huo wote, mtu alipofikia chungu ya vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia shinikizo apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu.

Soma pia kwa muda wako, Isaya 5:2, Hagai 2:16, Waamuzi 7:25, Nehemia 13:15, Ayubu 24:11, Isaya 63:3

SASA NENO HILI LINA MAANA GANI ROHONI?

Tukirudi katika kitabu cha Ufunuo tunaona, Yesu Kristo Bwana wetu, anajitambulisha kama yeye ndiye atakayekuwa mhusika mkuu wa  kukanyaga shinikizo la ghadhabu ya Mungu siku ile ya mwisho..

Ufunuo 19:15 “Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi”.

Yaani kwa lugha iliyo rahisi ni kuwa Bwana Yesu atakaporudi, yeye ndiye atakayetekeleza ile hasira ya Mungu ambayo alikuwa amehifadha kwa ajili ya watu wote waovu waliopo ulimwenguni leo hii.  Wakati huo unyakuo utakuwa umeshapita, mataifa yote yatamwombolezea siku atakaporudi, kutakuwa na mambo ya kutisha sana, kiasi mpaka biblia inatuambia, watu watatamani hata milima iwaangukie, ili tu wajiepusha na ghadhabu hiyo kali ya Mungu itakayoachiliwa duniani wakati huo, lakini halitawezekana ni lazima washiriki mapigo hayo (Ufunuo 6:16). Na ni Yesu ndiye atakayeitekeleza ghadhabu hiyo. Watu watakufa kama kumbikumbi, damu nyingi sana zitamwagika duniani..

Ufunuo 14:19 “Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.

20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili”.

KUPEWA KIKOMBE CHA MVINYO YA GHADHABU YA HASIRA YAKE.

Kipindi hicho sio cha kukitamani ndugu yangu.. SIKU YA BWANA INATISHA SANA,…Kwa urefu wa habari hizo fungua link hizi upitie ndugu ili ufahamu kitakachokwenda kutokea kwa watu wote watakaoukosa unyakuo leo >>

  1. KIAMA KINATISHA.
  2. MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Kimbuka kikombe hicho cha mvinyo wa ghadhabu ya Mungu, kila mwovu atakishiriki.

Ufunuo 16:19 “Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, KUPEWA KIKOMBE CHA MVINYO YA GHADHABU YA HASIRA YAKE.

20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.

21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno”.

Hivyo mimi na wewe, tuhakikishe, leo hii kuwa tupo upande salama, kwa kumpa Yesu maisha yetu ayaokoe, ndani ya kipindi hichi kifupi cha neema tulichobakiwa nacho. Upo wakati hatutaiona hii neema tuliyonayo sasa. Hivyo tubu, mgeukie Kristo. Hizi ni siku za mwisho.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

EPUKA MUHURI WA SHETANI

UFUNUO: Mlango wa 1

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nhalu bulugu
Nhalu bulugu
2 years ago

Nimejifunza jambo