JIBU: Ukisoma katika kitabu cha Kutoka, utaona kuna habari kama inajichanganya kuhusiana na baba-mkwe halisi wa Musa, Kwamfano Kutoka 2:18 Inasema aliitwa Reueli, lakini sehemu nyingine zote zilizosalia kama vile Kutoka 3:1,4:18, inamtaja kama ni Yethro. Je Kuna kuna makosa ya kiuandishi?
Embu tusome baadhi ya vifungu hivyo;
Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima. 16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao. 17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao. 18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo? 19 Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi. 20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula. 21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora.
Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.
16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao.
18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo?
19 Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.
20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula.
21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora.
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu”.
Jibu ni kuwa hakuna hitilafu, yoyote ya kiuandishi isipokuwa zamani ilikuwa ni jambo la kawaida mtu mmoja kuwa na jina zaidi ya moja, Kwamfano tukimtazama Yakobo, Mungu alimwambia utaitwa Israeli, Hivyo majina yake yote mawili utayakuta yakiandikwa sehemu mbalimbali katika biblia Lakini mtu ni Yule Yule mmoja.
Vivyo hivyo na Yethro mkwewe Musa, aliitwa pia Reueli, na kwasababu alikuwa ni kuhani, hatushangai kuona akiwa na majina mawili, moja la kwake la asili na lingine la kikuhani.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
Je Musa kumwoa Sipora, Mkushi alifanya dhambi?
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
Rudi nyumbani
Print this post