Neno kupiga kite limeonekana mara kadhaa katika biblia.
Maana ya “kupiga Kite” ni kutoa pumzi nje, kuashiria aidha kushangazwa, kupata unafuu au kukata tamaa.
Kwamfano mwanafunzi aliyekuwa anasubiria matokeo ya mtihani alioufanya, na wakati anaangalia matokeo kwenye orodha na kuona amefaulu basi unaweza kuona anashusha pumzi. (Kitendo hicho cha kushusha pumzi, kana kwamba kapunguza presha ndani yake, kitendo hicho ndicho kinachoitwa kupiga Kite).
Au mtu aliyejaribu kufanya jambo fulani kwa muda mrefu, asifanikiwe na kuazimia kujaribu kwa mara moja ya mwisho, kama tumaini lake la mwisho, na wakati anangojea kupata tumaini zuri, ghafla yanakuja matokeo mabaya ya kuvunja moyo, mtu wa namna hiyo pia utaona anashusha pumzi, kuashiria kukata tamaa (kitendo hicho pia ni kupiga kite).
Limetumika neno “kupiga” na sio “kufanya”...kwasababu matendo hayo ya kuvuta pumzi au kutoa, yanatamkwa kwa kuanza na neno “kupiga”..kwamfano “kupiga miayo”, huwezi kusema “kufanya miayo”.
Katika biblia Neno hilo limeonekana mara kadhaa.
Maombolezo 1:11 “Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamaniko yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge”.
Pia,
Maombolezo 1:4 “Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu”.
Unaweza kusoma pia 9, utaona Neno hilo hilo.Unaweza kusoma pia Maombolezo 1:21, na Zaburi 90:9 , utaona Neno hilo hilo.
Je umemwamini Bwana Yesu?..kumbuka ulimwengu huu unapita na mambo yake yote, miaka yetu inapukutika kama kite, anaanza na matumaini inaishia na huzuni na kukata tamaa, lakini kama tukiwa ndani ya Yesu itaanza na huzuni lakini itaishia na furaha.
Zaburi 90:9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
TAFUTA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KWA HUDUMA MUNGU ALIYOIWEKA NDANI YAKO.
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
Rudi nyumbani
Print this post