SWALI: Isaya 59:5 ina maana gani?
Isaya 59:5 Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
JIBU: Ni mstari unaoeleza asili ya watu waovu.
Anasema huangua mayai ya fira. Fira ni aina ya nyoka wenye sumu kali sana, ambao kwa kawaida mtu akikutana nao, ni lazima awaue, au akikuta mayai yao ni lazima ayakanyage, kwasababu, asipofanya hivyo yakitotolewa wataleta madhara, Lakini mtu mwovu biblia inasema ni kinyume chake huyatotoa. Ikiwa na maana ni mtu ambaye anaona madhara Fulani yanakuja mbele kwa wengine badala ayaangamize, yeye ndio anayekuwa wa kwanza kuyakumbatia.
Mfano mmojawapo wa hawa ni manabii wa uongo, wanaojua kabisa, dhambi ina madhara, na mtu asipoishi katika utakatifu hawezi kumwona Mungu (Waebrania 12:14), lakini kwasababu hawataki kupoteza watu, kwa tamaa za pesa, hawawaonyi juu ya mambo kama hayo, kinyume chake ndio wanawasogeza kabisa kwenye mambo ya mwilini, biashara na mali, wanamsahau Mungu. Halafu wanakufa katika dhambi zao na kwenda kuzimu.
Vilevile anasema husuka wavu wa buibui. Kama vile tunavyojua buibui anaposuka wavu wake, ni kwa lengo la kunasa wadudu awale. Halikadhalika asili ya watu wa waovu ndivyo ilivyo, huandaa mazingira yote, ya wenzao kunaswa katika mambo maovu na kuangamia.
Kwamfano unapomwombea adui yako afe, ni sawa na mtu anayeunda wavu wa uangamivu. Bwana alisema tuwaombee, lakini sisi tunawatakia mauti, tena katika maombi.
Kwa ufupi, hii ni tabia ya kutengeneza kama sio kufurahia anguko la wengine.
Hivyo biblia inatuonyesha pia tukiwa na tabia kama hizo, zinatufanya na sisi Mungu asitutee na kutupa haki zetu kwa vile tumwombavyo, nasi majibu yanakuja kinyume chake.. Pale tunapotazamia jema linakuja ovu,na tunapotazamia nuru linakuja giza, tunalithitibitisha hilo katika vifungu vinavyofuata..
Isaya 59:6-9
6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao. 7 Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao. 8 Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani. 9 KWA SABABU HIYO HUKUMU YA HAKI I MBALI NASI, WALA HAKI HAITUFIKILII; TWATAZAMIA NURU, NA KUMBE! LATOKEA GIZA; TWATAZAMIA MWANGA, LAKINI TWAENDA KATIKA GIZA KUU.
6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.
7 Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao.
8 Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.
9 KWA SABABU HIYO HUKUMU YA HAKI I MBALI NASI, WALA HAKI HAITUFIKILII; TWATAZAMIA NURU, NA KUMBE! LATOKEA GIZA; TWATAZAMIA MWANGA, LAKINI TWAENDA KATIKA GIZA KUU.
Hivyo tupambane, kwa bidii zote tusiwe vyombo vya shetani vya kuunda mabaya kwa wengine.
Bwana atusaidie.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Injili iliyopo kwa Samaki aina ya Eeli.
Lumbwi ni nini katika biblia?
Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
Donda-Ndugu ni nini?
Rudi nyumbani
Print this post