Haya ni maswali 8 maarufu yahusuyo Zaka.
1. Ni nani anayepaswa kutoa fungu la 10?,
2. Je fungu la 10 tunatoa katika faida au mtaji?
3. Je tunapopewa zawadi tunazitolea fungu la 10?,
4. Je fedha ya mkopo inatolewa fungu la 10?.
5. Je Kama mshahara wangu ni milioni moja lakini kutokana na makato ya serikali kama kodi, na pspf, najikuta napokea sh.laki 7 tu, je zaka natoa kutoka katika hiyo laki 7 au kutoka katika ile milioni.?
6. Je kama nimepokea mshahara ambao haupo katika mfumo wa kifedha, mfano napewa ng’ombe au kuku, namtoleaje zaka huyo?
7. Je!. Tunaweza kuweka deni la fungu la 10? Yaani badala ya kutoa.kila.siku, tukakusanya na hatimaye tukaja kulipa mwisho wa mwezi au mwaka?
8. Je! Fungu la 10 linapaswa lipelekwe wapi kimaandiko?.Na je kuna ulazima wowote wa kulipa zaka?
Tukianza na swali la kwanza.
1. Ni nani anayepaswa kutoa fungu la 10?(Zaka).
Jibu: Kila mtu aliyeokoka ana wajibu wa kutoa fungu la 10. Haijalishi umri wake, jinsia yake?, au hali yake ya kiuchumi.
Maana yake kama unafanya kazi ya mikono au haufanyi, ni lazima kutoa fungu la 10 (yaani kulipa zaka).
2. Fungu la 10 tunatoa katika faida au mtaji?
Fungu la 10 linatolewa katika faida na si mtaji. Mfano una mtaji wa laki moja, na kazi unayoifanya imakupa faida kwa siku sh. Elfu kumi. Hapo zaka utatoa kutoka katika hiyo faida uliyoipata na si. Kutoka katika mtaji ulionao (maana yake kiasi cha zaka unachopaswa utoe hapo kwa siku ni sh. Elfu moja).
3. Je tunapopewa zawadi tunazitolea fungu la 10?
Kama zawadi hiyo uliyopewa utaifanya kuwa mtaji, basi hutaitolea zaka, lakini utatoa katika faida huo mtaji utakayoizalisha. Lakini kama zawadi hiyo matumizi yake ni kama ya mshahara wa kawaida..yaani katika kujihudumia kwa chakula, makazi au malazi, basi utaitolea zaka.
Na vile vile kama hufanyi kazi yoyote, au bado hujapata kazi, chochote kitakachofika mkononi mwako kwaajili ya mahitaji yako, hicho utakitolea zaka.
4. Je fedha ya mkopo, tunaitolea zaka?
Kama mkopo uliochukua ni kwa lengo la mtaji wa biashara, hupaswi kuutolea zaka, bali utatoa zaka katika faida utakayoipata kutoka katika mkopo huo.
Lakini kama mkopo ulioupokea ni kwa lengo la kujihudumia kimaisha kama chakula, mavazi au malazi (Huo ni kama mshahara, hivyo unapaswa uutolee zaka).
5. Kama mshahara wangu ni milioni moja lakini kutokana na makato ya serikali kama kodi, na pspf, najikuta napokea sh.laki 7 tu, je zaka natoa kutoka katika hiyo laki 7 au kutoka katika ile milioni moja.?
Jibu: Zaka utatoa kutoka katika hiyo milioni moja na si kutoka katika hiyo laki 7, maana yake kiasi cha zaka hapo kitakuwa ni sh. Laki moja kila mwezi.
6. Je kama nimepokea mshahara/Zawadi ambayo haupo katika mfumo wa kifedha, mfano napewa ng’ombe au kuku, namtoleaje zaka huyo?
Jibu: Kama ng’ombe huyo utamfanya kuwa mtaji, hautamtolea zaka, isipokuwa faida utakazozipata kutoka katika shughuli hiyo, utaitolea zaka (maana yake kama utafanya biashara ya kuuza maziwa, faida utakayoipa kupitia maziwa hayo, utalipa zaka).
Lakini kama utamtumia kwaajili ya kitoweo, hapo huna budi kutafuta thamani ya ngombe huyo na kutoa sehemu ya 10, maana yake kama ng’ombe ana thamani ya milioni moja basi utatoa laki moja kama zaka, au kama hutaweza kupata thamani hiyo, basi utaitoa sehemu ya 10 ya nyama kama zaka.
7. Je!. Tunaweza kuweka deni la fungu la 10? Yaani badala ya kutoa kila siku, tukakusanya na hatimaye tukaja kulipa mwisho wa mwezi au mwaka mwaka?
Jibu: Ndio! Lakini kama kuna ulazima wa kufanya hivyo. Mfano unaweza ukawa unapata faida ndogo, ambayo mahesabu ya zaka yake yanakuwa ni chini ya sh.50, sasa huwezi kutoa sh 40 au 20 au 10 kama zaka kila siku, kwasababu hata matumizi ya hizo sarafu hayapo!.Kwahiyo suluhisho ni kufanya mahesabu ya kiasi kinachopatikana kwa wiki au mwezi, na kulipa kwa pamoja.
Vile vile hakuna ratiba maalumu ya kimaandiko ya wakati wa kulipa zaka..maana yake kama mtu atachagua kulipa kila mwisho wa wiki, hafanyi dhambi, mwingine kila mwisho wa mwezi hakosei, mwingine kila mwisho wa miezi mitatu pia afanyi makosa, ilimradi analipa kiasi chote kwa uaminifu. (Lakini ni vizuri zaidi kulipa mapema, ili kuzuia mlundikano wa madeni..lakini kila mtu anao ustaarabu wake, ambao yeye anauwezo wa kuumudu).
8. Je fungu la 10 linapaswa lipelekwe wapi?..kwa mayatima, kanisani, kwa mtumishi wa Mungu au wapi?.
Ili kupata kupata jibu la swali hili kwa urefu unaweza kufungua hapa >>>> NI WAPI MAHALI SAHIHI PA KULIPA ZAKA?
Bwana atubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE! KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KULIPA ZAKA?
Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
About the author