Kusubu ni nini? Miungu ya kusubu ni ipi?

Kusubu ni nini? Miungu ya kusubu ni ipi?

Kusubu kibiblia ni kitendo cha kuyeyusha dhahabu au  fedha au ‘kito’ chochote kwa lengo la kuunda kitu kingine kipya.

Neno hilo utalisoma sehemu nyingi katika biblia kwa mfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakutana nalo;

Mambo ya Walawi 19:4

[4]Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

Maana yake msaifanye sanamu za kuyeyusha,

Kumbukumbu la Torati 27:15

[15]Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.

Soma pia..

2Nyakati 24:4, 28:2, Waamuzi 17:3, Hesabu 33:52, 1Wafalme 7:23.

Maana yake ni ipi kiroho?

Hata sasa watu wengi, wanajiundia sanamu zao za kusubu rohoni bila wao kujijua…kwa kugeuza maumbile ya vitu vyema na kuvitumia isivyopasa..mpaka kuviabudu.

Kwa mfano fedha si mbaya lakini leo hii watu wameigeuza fedha kuwa mungu wao..kiasi kwamba kwao Mungu si kitu zaidi ya fedha, maisha yao yote ni kuhangaikia mali, kana kwamba hiyo ndio itakayowafikisha mbinguni, kaacha kumtumikia Mungu, hata muda na ibada hana, dai lake ni “Natafuta pesa’’ Sasa hizo ndio sanamu za kusubu..

Wengine biashara kwao zimeshageuka na kuwa sanamu za kusubu, wengine wanadamu., wengine muvi, wengine magemu, wengine mipira.

Tunapaswa tujilinde sana kwasababu sanamu za namna hii zinamtia Mungu WIVU, na wivu ni mbaya kuliko ghadhabu..

Ni heri Mungu akukasirikie kwa makosa mengine kuliko kwa kukuonea wivu.

kwasababu adhabu ya wivu ni mbaya sana kuliko ya hasira..

Mithali 27:4

[4]Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika;

Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.

Tujilinde mioyo yetu na ibada za sanamu. Mungu hakuwahurumia wana wa Israeli walipotengeneza ndama ya kusubu na kuiabudu kule jangwani. Japokuwa yeye ndiye aliyewaokoa kwa mkono hodari.

Vivyo hivyo na wewe ukisema umeokoka, epuka kugeuza kitu chochote kuwa Mungu wako. Usiruhusu kamwe chochote kuchukua sehemu ya Mungu yako.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)

Shetri ni nini kama tunavyosoma katika Marko 3:38?

Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).

Zeri ya Gileadi ni nini?

Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Leonard Lume
Leonard Lume
4 months ago

Napenda sana mafundishi yenu watumishi wa mungu, mbarikiwe sana