Biblia inasema..
1 Wakorintho 2:10-12
[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
[11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
[12]LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA, BALI ROHO ATOKAYE KWA MUNGU,makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
Zipo Roho mbili tu huku duniani.
Roho wa Mungu, na roho ya dunia. Kama mtu usipoipokea Roho ya Mungu, basi utaipokea roho ya dunia.
Hakuna mwanadamu anayejiongoza yeye mwenyewe hapa duniani kwa roho yake tu. Hilo halipo.
Sasa kama jinsi hayo maandiko yanavyotuambia Roho wa Mungu huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu.. Maana yake ni kuwa yeye ndiye anayetufunulia siri za ufalme wa mbinguni, pamoja mambo ambayo Mungu anataka sisi tuyafanye tukiwa hapa duniani..ukisoma Yohana 16:13 inasema
[13]Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Umeona hiyo ndio kazi ya Roho wa Mungu..ndio maana mtu aliyepokea kweli Roho Mtakatifu hawezi ishi kidunia kwasababu ni roho nyingine kutoka mbinguni kwa baba ipo yake ikimfundisha kuishi kulingana na misingi ya Mungu.
Lakini kinyume chake ni kweli. Watu wote ambao hawana Roho wa Mungu, wanayo roho ya dunia
Na yenyewe inachunguza mambo ya ulimwengu huu na kuwafundisha watu kuishi kiulimwengu. Ndio maana hushangai kuona tabia nyingi mbaya kila siku zikivumbiliwa lengo tu ni kuwafanya kuwa wakidunia.
Ukiona mwanamke unapenda fashion, vimini, kujichubua, unavaa suruali, unaweka mak-eups, kijana unavaa milegezo, unanyoa viduku, unakunywa pombe, unacheza kamari, unasikiliza nyimbo za kidunia, unakwenda disco, unafanya ushirikina, unazini, unakula rushwa, unaiba, unapenda fedha, unadanganya ni uthibitisho kuwa roho ya dunia imekuvaa ndio maana inakuhimiza na kukufundisha kufanya hayo mambo kwa bidii.
Na mwenye roho hii ni shetani mwenyewe..Na kama ikitokea Bwana Yesu amerudi leo..basi ujue utabaki hapa duniani. Kwasababu roho yako ni ya hapa hapa na ka ikitokea umekufa basi utaenda moja kwa moja kuzimu kwasababu huko ndiko hatma ya roho hiyo itakapoishia..
Biblia ipo wazi kabisa inasema..
Warumi 8:9
[9]Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. LAKINI MTU AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA ROHO WA KRISTO, HUYO SI WAKE.
Ukikosa Roho wa Mungu, mbinguni huendi. Huu si wakati wa kumvumilia zaidi shetani, au kuwa rafiki wa dunia. Tunapojichanganya na mambo yake ndipo tunapovaliwa na roho hii chafu. Jiponye nafsi yako, ndugu, hizi ni siku za mwisho.
1 Yohana 2:15
[15]Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Hivyo ndugu, njia pekee ya kuipokea Roho ya Mungu ambayo itakusaidia na kukufundisha kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Ni kutubu kwa kumaanisha kabisa kugeuka na kuuacha ulimwengu..kisha ukishafanya hivyo unakuwa tayari kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo ikiwa kama haukubatizwa hapo mwanzo.
Baada ya huo wakati ni kuanza kuonyesha bidii ya kujifunza biblia, kuomba, kuzingatia fellowship zitakazokusaidia kukua kiroho. Na Roho wa Mungu akishaona umemaanisha hivyo, atashuka juu yako na kukutia Muhuri, na kukusaidia kuishi maisha ya wokovu.
Huku ukingojea siku yako ifike uende mbinguni, Roho hiyo ilipo.
Ikiwa utahitaji msaada ya kupokea wokovu, àu ubatizo sahihi.Basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi
+255693036618/ +255789001312
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizo
Mada Nyinginezo:
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.
Kusubu ni nini? Miungu ya kusubu ni ipi?
Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?
TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?
About the author