Yapo maombi ya namna tofauti tofauti, lakini yote ni lazima yaangukie katika mojawapo ya makundi haya Matano (5).
Wengi hawafahamu kama sifa zetu ni maombi yanayojitegemea kwa Mungu, haya ni maombi yanayomwasilia Mungu katika mfumo wa nyimbo, halikadhalika pia kwa kumwadhimisha kwa matendo yake makuu aliyoyafanya kwa kuzungumza kwa vinywa vyetu.. ndio maombi ya kwanza yenye nguvu. Tunapomsifu Mungu katika Roho na kweli, ni Zaidi ya maombi mengine yote tunayoweza kuyapeleka kwake.,
Biblia inasema Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu;(1Nyakati 16:29), Na pia Mataifa yote yamsifu yeye. Mambo mengi, na vifungo vingi huwa vinafunguka, pale tu tunapomsifu Mungu kwa kumaanisha katika Roho na kweli, Kwasababu ni maombi yanayouvuta uwepo wa Mungu kwa haraka sana juu ya mtu, Na ndio maana ibada zote lazima zitanguliwe na maombi haya.
Ni maombi ya kuwaombea wengine, Zaidi ya kwako mwenyewe. Kuwaombea watakatifu, kuwaombea, wanyonge, kuliombea taifa, viongozi, hata maadui zako n.k. Haya ni maombi ambayo yanampendeza Mungu sana. Danieli alifunga na kuomba kwa ajili ya taifa lake Israeli, na dhambi zao, Na Mungu akamsikia akamrehemu (Danieli 9:1-27).
Bwana Yesu alipokuwa duniani, sehemu kubwa ya maombi yake ilikuwa ni kutuombea sisi (Yohana 17) hivyo akasema pia, tuombeane sisi kwa sisi ili tupate kuponywa (Yakobo 5:16). Ikiwa na maana wengi hawawezi kuokoka/kufunguliwa wenyewe, ikiwa sisi hatutawaombea, Na pale maombi haya yanapokuwa ya muda mrefu (ya dua), basi huwa yana nguvu Zaidi, kupelekea kutupa kibali cha kupendwa na Mungu, kama ilikuwa kwa Danieli.
Ni maombi ya kupeleka haja zetu kwa Mungu, ikiwemo, kumwomba Roho wake, rizki, amani, furaha, uponyaji, kibali, fursa, gari n.k. Bwana Yesu alisema pia, tuombapo tuombe Bwana atupe rizki zetu,(Mathayo 6:11). Na pia alisema tuombe nasi tutapewa. Haya ndio maombi yanayojulikana na kuombwa na watu wengi sana.
Luka 11:11 “Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?
12 Au akimwomba yai, atampa nge?
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”
Ni maombi muhimu kwa kila mwanadamu, ni maombi ya wakati wote, ya asubuhi, ya mchana, na jioni, tunamshukuru Mungu, kwa uhai, afya, chakula, makazi, Malazi, familia,
Wakolosai 3:15 inasema “….tena iweni watu wa shukrani.”. Ulishawahi kushukuriwa kwa wema Fulani uliomtendea mtu, ukaona hali unayojisikia ndani ya moyo wako kwa shukrani ile..Ndivyo ilivyo kwa Mungu anapoona Sio kila majira tunaenda kumpelekea tu mahitaji yetu..Bali wakati mwingine tunamkaribia kumshukuru kwa vile anavyotufanyia. Inampendeza sana moyo. Na wakati mwingine kupelekea hata kupewa vile vilivyosalia, kwasababu tunaonyesha kuthamini neema yake.
Ni maombi ya kushindana, na nguvu za giza, kwa mamlaka ya rohoni tuliyopewa katika damu ya Yesu, Hapa tunatangaza ushindi, na pia kutamka kwa Imani katika Neno la Mungu. Yapo mambo mengine ibilisi hawezi kuyaachia kirahisi rahisi. Hivyo inahitaji kukemea, kuamuru, kuvunja, na kubomoa, kwa Imani.
Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa”.
Hivyo kama watakatifu tukijifunza kutumia aina hizi tano za maombi, bila kupuuzia hata moja, basi, tutakuwa ni askari wazuri sana katika roho.
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
WALA TUSIACHE KUKUSANYIKA PAMOJA
LAKINI SISI HATUKUIPOKEA ROHO YA DUNIA.
About the author