MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAENEO YA IBADA: Sehemu ya 1
KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.
Kuna mambo ambayo yanaonekana madogo, lakini yana madhara makubwa sana rohoni. Watu hawafahamu kuwa wanaweza kufa kabisa kiroho kwa tabia ya kuendekeza USINGIZI ibadani..
Embu tusome habari ya Eutiko, tuone ni jambo gani Bwana anataka tufahamu nyuma ya matukio yaliyokuwa yanaendelea pale..
Tusome.
Matendo ya Mitume 20:7-10
[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
[8]Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika.
[9]Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
[10]Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake.
Nataka tuyatathimini hayo mazingira..kwanza walipokuwa wanasilizia injili ni katika gorofa, na gorofa yenyewe si ya kwanza bali ni ya tatu..
Pili japokuwa mahali pale ilikuwa ni usiku lakini biblia inatuambia kulikuwa na taa nyingi sana..maana yake ni kuwa mazingira yote yalikuwa yanaonekana, yapo wazi hivyo mahali pa hatari palionekana, na mahali salama pia palionekana.
Lakini tunaona huyu Eutiko alichagua kwenda kukaa katika dirisha la gorofa, akijua kabisa mahali pale si salama kukaa endapo akiteleza kidogo na kuanguka..
Lakini hakujali hilo, baada ya muda kidogo akasinzia.. Na matokeo yake akaanguka kutoka katika ile gorofa ya tatu. Na alipofika chini alikuwa tayari ameshakufa..
Ni kwanini habari hii iandikwe hapa? Kumbuka kila hadhithi inayoandikwa katika biblia inafundisho kubwa sana nyuma yake.
Sasa kitendo cha kuwepo katika gorofa ya tatu.
Inamaanisha kuwa mahali popote Neno la Mungu, linahubiriwa, au ibada inaendelea, iwe ya jumapili, au fupi ya maombi au mikesha, Rohoni mnakuwa mmechukuliwa mpaka mbingu ya Tatu (ndio ile gorofa ya tatu), juu sana mahali ambapo Mungu yupo na kiti chake cha enzi kilipo.
Na huko kuna Nuru nyingi, kama tulivyoona jinsi taa nyingi zilivyokuwa pale gorofani. Ikiwa na màana kuwa wakati unajaribu kuchagua kusogea mbali na uwepo wa Mungu utatambua kabisa mahali ulipo si salama..
Tabia ya kusinzia inakutuma ukae dirishani mwa uwepo wa Bwana na sio ukumbini. Ni kuonyesha jinsi gani usivyo “siriazi” na Mungu.
Na hatimaye unaanguka kutoka uweponi mwa Bwana..na kufa moja kwa moja kiroho.
Leo imekuwa ni desturi na mtu/watu wengi kila wafikapo nyumbani kwa Mungu ni lazima wasinzie, na wenyewe wanaona ni kawaida, wanadhani pale ni sawa na ofisini kwao, au shuleni kwao, ambapo hakuna jambo lolote la rohoni linalokuwa linaendelea.
Wanasahau kuwa wamepewa neema ya kupandishwa hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu, lakini wanakaa madirishani.
Ndugu ikiwa wewe ni mmojawapo wacha hii tabia, ukiindekeza utaanguka na kufa kabisa kiroho. Nimeona watu wengi wenye tabii hii, wakirudi nyuma ulimwenguni, wengine wakichuliwa na mawimbi ya ibilisi.
Kuwa siriazi na Mungu wako, tambua kilichokupeleka pale, unapoona wengine hawasinzii, haimaanishi kuwa hawahisi usingizi kama wewe, wanahisi lakini watalalaje mbele ya kiongozi wao mkuu? Wanaogopa kumvunjia heshima yake. Vilevile wanataka wapokee kikamilifu kile kilichowapeleka pale,
Hivyo kataa usingizi na wenyewe utakukimbia, na hiyo inakuja kwa kuzingatia kwa makini kile kinachoendelea pale, mawazo yako yote yakiwa pale, ukijua kabisa kila siku ni mpya nyumbani kwa Bwana, na Mungu anatembea.
Lakini kama utaenda kwa desturi na mazoea, au kukamilisha ratiba, utakuwa ni mtu wa kulala lala na siku moja utakufa kabisa kiroho kwasababu uwepo wa Mungu umekwisha kukuacha. Mheshimu Mungu.
Bwana atasaidie sana.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
About the author