Luka 23:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura”
Je umeshawahi kumwombea msamaha mtu aliyekufanyia ubaya?.
Wengi wetu huwa tunaweza kusamehe tu, lakini tukaishia kusema “namwachia Mungu”. Tukiwa na maana kuwa Mungu ndiye atakayeshughulika na huyo mtu au hao watu na sio sisi.
Ni kweli, si vibaya kuwa mtu wa kusamehe na kumwachia Mungu, ashughulike na yaliyosalia, lakini msamaha wa namna hiyo hauumfanyi mtu kuwa mkamilifu.
Msamaha mkamilifu ni ule wa wewe kusamehe, na pia kumwombea msamaha kwa Baba yule aliyekukosea.
Bwana Yesu aliwasamehe wale wote waliomsulubisha, wale wote waliomtemea mate na kumpiga mijeledi, lakini pamoja na kwamba aliwasamehe yeye binafsi, pia alijua msamaha wake yeye binafsi hautoshi, kuwacha wale salama..alijua bado ghadhabu ya Mungu ilikuwa juu yao, hivyo akamwomba pia Baba asiwaadhibu, na Baba akawasamehe. (Huo ndio msamaha mkamilifu).
Ndugu Ukiteswa na kudhalilishwa, kwanza samehe wewe mwenyewe na kisha mwombee msamaha kwa Baba yule anayekufanyia huo ubaya.,
Ukidhulumiwa msamehe yule aliyekudhulumu kisha mwombee msamaha pia kwa Mungu, usiishie kumsamehe tu.(Kwasababu hajakuudhi tu wewe, amemuudhi pia na Mungu, hivyo mwombee msamaha kwa Mungu pia).
Ukipigwa msamehe yule aliyekufanyia huo ubaya na kisha mwambie pia Bwana amsamehe.
Tukiwa watu wa aina hiyo, basi tutakuwa wakamilifu kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa mkamilifu, na kwasababu hiyo ndio tutaitwa waKristo.
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,…………48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,…………
48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NENO LA MUNGU NI UFUNUO MKAMILIFU.
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
NINI MAANA YA KUTUBU
Je wale waliomsulubisha Bwana, wataenda mbinguni, kwakuwa walisamehewa?
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Rudi nyumbani
Print this post