Swali: Pale Forodhani, Mathayo alipokuwa ameketi ndio mahali gani? (Mathayo 9:9).
Jibu: Tusome,
Mathayo 9:9 “Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona MTU AMEKETI FORODHANI, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata”
“Forodha” ni “Nyumba au kijumba kidogo” kinachotumika kukusanyia mapato.. Kwamfano watu wanaofanya kazi benki, huwa wanaketi ndani ya madirisha Fulani maalumu ya kupokea au kutoa fedha, sasa vyumba vile walivyopo ndivyo vinavyoitwa “forodha” ( kwa lugha nyingine).
Hali kadhalika watu wanaofanya kazi katika mashirika ya kukusanya mapato, huwa wanaketi katika chumba maalumu chenye dirisha ambapo wanapokea fedha na kutoa risiti. Vyumba hivyo ambavyo vimetengenezwa mahususi kwaajili ya kupokea wateja na kodi zao, au ada zao, au ushuru wao ndivyo vinavyoitwa Forodha.
Katika siku hizi Forodha pia zinatengenezwa na wafanya biashara, kutokana na kutanuka kwa wigo wa kibiashara, kwamfano watu wanaofanya kazi za uwakala wa mitandao ya simu mf. Mpesa n.k huwa wanatengeneza Viforodha vidogo, kwaajili ya shughuli zao hizo za kutoa na kupokea fedha.
Lakini ni funzo gani tunalipata kwa Mathayo aliyeketi Forodhani?..
Mathayo alipoitwa na Bwana Yesu, muda ule ule aliitikia wito!, hakungoja kesho, wala baadaye, badala yake muda ule ule alimfuata Bwana YESU.. Ijapokuwa alikuwa yupo katika mazingira magumu ya kumfuata Bwana Yesu, lakini ilimgharimu kuacha vyote na kumfuata Yesu!. Na faida ya kumfuata Yesu, Mathayo pamoja na wenzake waliyoipata, ni kwamba walikuja kupata mara mia kwa vile vyote walivyovipoteza, na zaidi sana walipata ahadi ya uzima wa milele.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.
Mathayo 19:27 “Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi?
28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli”.
Je ni kazi yako ndio kikwazo cha wewe kumfuata Yesu?, je ni watoto wako au mke wako au wazazi wako ndio kikwazo cha wewe kumfuata Yesu kwa moyo wako wote na nguvu zako zote?.. kama kazi yako ndio kikwazo, basi nataka leo umkumbuke Mathayo, yeye kazi yake aliona si kitu zaidi ya wito wa Mungu!. Na mwishowe leo hii tunasoma waraka wake huu.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
Rudi nyumbani
Print this post