Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?

Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa?

SWALI: Je huduma za mitume na manabii, zinaendelea kufanya kazi hadi sasa? Kwani kunaendelea mabishano baina ya wakristo baadhi, wengine wanasema kwasasa huduma hizo hazitendi kazi tena kufuatana na andiko la Paulo katika

Waefeso 2:20 linalosema; 

[20]Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

…Lakini wengine wanasema huduma hizo hadi sasa zipo katika kanisa. Je ukweli ni upi?


JIBU: Kabla hatujafahamu kwanza kama huduma za mitume na manabii zinaendelea hadi sasa au la!…tutazame kwanza aina za manabii wa mwanzo, na mitume wa mwanzo walikuwaje..

Manabii wa zamani walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. 

1)Manabii wa kutia msingi wa wakati wote

2)Manabii wa kuthibitisha misingi.

1 ) Hawa manabii wa kutia misingi; Ndio wote waliotiwa mafuta na Mungu kaandika biblia takatifu…mfano wa hawa ndio kama  Yeremia, Isaya, Nahumu, Malaki, Yoeli, Yona, Habakuki..n.k. Kwamba nabii zao zisimame kama msingi na mwongozo wa daima wa kuliongoza kanisa la Mungu wakati wote.. 

2 ) Manabii wa kuthibitisha: Hawa Mungu aliwanyanyua kutoa mwongozo wa wakati fulani tu mahususi.. Walikuwa wanasema Neno la Mungu lakini la wakati fulani tu ambapo ukishapita basi, unabii huo hauna umuhimu tena kwa vizazi vijavyo.

Mfano wa hawa utawasoma wengi sana..wakina Mikaya, Aguri, Odedi, Azuri,  Ahiya, pia katika agano jipya walikuwepo wakina sila, agabo..n.k

Vivyo hivyo tukirudi na  katika Mitume wa Kristo.

Wapo ambao waliotiwa mafuta kwa lengo la kuweka misingi ya daima. Hawa ndio wote tunaosoma nyaraka zao katika maandiko..mfano Paulo, Petro, Yakobo, Yohana, Yuda,  Mathayo, Luka.

Na wapo waliowekwa kwa ajili ya kutihibitisha / kutia misingi midogo.midogo. Mfano wa hawa ni Epafrodito Wafilipi 2:25..

Sasa tukishafahamu…hilo…tunaporudi katika lile andiko linalosema..mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii tunaweza kuelewa

Tusome; 

Waefeso 2:20

[20]Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

Maana yake ni kuwa sisi kama kanisa tumejengwa juu ya mafunuo ya manabii watangulizi na mitume watangulizi wale waliochaguliwa kuweka misingi ya daima..(Yaani kwa lugha rahisi tumejengwa juu ya  BIBLIA TAKATIFU)…

Hakuna namna tutajengwa juu ya misingi mingine mipya zaidi ya hiyo yao.. Hivyo kwasasa hatuna manabii na mitume kama wale watangulizi, ambao walipokea mafunuo ya moja kwa moja ya namna ya  kulijenga kanisa la Kristo..ni sawa na kusema hatuna mitume mfano wa Paulo au Petro au manabii mfano wa Yeremia au Isaya, kwasasa.

Lakini wapo mitume na manabii wa nyakati ndogo ndogo, ambao wanafanya kazi za kuthibitisha misingi ambayo tayari ipo lakini sio wa kuleta jambo jipya duniani..

Kwamfano kazi mojawapo ya mitume ilikuwa ni kwenda kupanda makanisani mapya maeneo mapya..hivyo, mtu yeyote mwenye huduma.hii ndani yake, ni mtume lakini kazi yake itakuwa ni kutembea katika mstari ule ule wa mitume wa kwanza..hapaswi kuja na jambo lake jipya..anapaswa ahubiri kilekile mitume walichokifundisha, hapo atakuwa amekidhi kuitwa mtume.

Ni sawa na mtu anayejenga nyumba ya gorofa..msingi mkuu ni mmoja..ule uliopo chini…lakini akitaka aweke nyumba juu yake ni sharti afuata ramani ya msingi wa chini….

Ndivyo ilivyo kwa huduma hizi za kitume na kinabii.. Ni lazima zirejee katika biblia takatifu chochote kitolewacho lazima kionekane katika biblia sio katika maono yao wenyewe wanayojitungia.

Paulo aliandika maneno haya; 

1 Wakorintho 3:10-15

[10]Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

[11]Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.

[12]Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri.

[13]Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.

[14]Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.

[15]Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.

Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa tofauti ya wale na hawa ni kwamba wote kazi yao ni moja ya upandaji wa kanisa la Kristo,mahali na mahali, isipokuwa wasasa hawaleti fundisho jipya, au maono mapya isipokuwa yale ambayo tayari yameshaanzishwa na mitume.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Nitamjuaje nabii wa Uongo?

JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?

Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?

Hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.

JINSI MTUME PAULO ALIVYOUTHAMINI WITO WAKE, JUU YA WENYE VYEO.

VIFO VYA MITUME WA YESU/ JINSI MITUME WALIVYOKUFA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments