MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!.

MAHANAIMU (Jeshi la Mungu)!.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu…

Yakobo baada ya kuondoka kwa Labani, alipokuwa njiani maandiko yanasema alikutana na Jeshi la Malaika wa Bwana…

Mwanzo 32:1 “Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye. 

2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, MAHANAIMU”.

Maana ya Neno “Mahanaimu” ni “Kambi mbili”…Yakobo alipaita mahali pale kwa jina hilo, kwasababu kaliona jeshi la Bwana likiwa pamoja naye..  Na hivyo kufanya jumla ya majeshi Mawili; jeshi lake yeye mwenyewe (yaani yeye na watumishi wake na watu wake wote) na la Bwana (malaika watakatifu).

Baada ya kuona jeshi hilo la Mbinguni likifuatana naye, ndipo alipojua kuwa hayupo mwenyewe, hivyo nguvu mpya na hofu yote ikamwondoka, Na hofu ya kwanza ambayo ilikuwa inamsumbua kwa muda mrefu ni ile ya kukutana na ndugu yake Esau, maana alikiri kabisa mwenyewe kuwa anamwogopa ndugu yake Esau (Mwanzo 32:11).

Lakini baada ya kujua kuwa lipo Jeshi lingine kubwa la mbinguni linamzungukan na kufuatana naye, ndipo akapata ujasiri mpya na kuamua kumtafuta ndugu yake..

Mwanzo 32:1 “Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.

2 Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu.

3 Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu

4 Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa, 

5 nami nina ng’ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako.

6 Wale wajumbe wakarudi kwa Yakobo wakisema, Tulifika kwa ndugu yako, Esau, naye anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye”.

Jambo kama hilo hilo lilitokea pia kwa Elisha, kipindi Mfalme wa Shamu alipotuma majeshi kwenda kumkamata Elisha pamoja na mtumishi wake, walipoamka asubuhi Elisha na mtumishi wake waliona jeshi la Washami limezunguka lile eneo lote.. Na Yule mtumishi wa Elisha akaishiwa nguvu kwa hofu, lakini Bwana akamfumbua macho na kuona jeshi kubwa la Malaika  wa mbinguni, lililo kubwa kuliko jeshi la Washami limezunguka kile kilima chote..

2Wafalme 6:15 “Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? 

16 Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. 

17 Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote”.

Jeshi hilo hilo pia limewazunguka leo watu wa Mungu(Waliompokea Yesu),  wakati mwingine unaweza kuwa na hofu na kudhani Mungu hayupo na wewe, hata Yakobo alidhani hivyo, hata Mtumishi wa Elisha alidhani hivyo.. Lakini hawakujua kuwa lilikuwepo  jeshi lingine kubwa la mbinguni lililofuatana nao, kuhakikisha kuwa wanafanikiwa katika njia zao.

Leo hii unaweza usifumbuliwe macho kama Mtumishi wa Elisha au kama Yakobo, lakini amini kuwa lipo jeshi lingine  kubwa sana la mbinguni limekuzunguka.. hivyo usiogope siku zote kuendelea mbele, wala usiogope maadui…

Yakobo alimwogopa ndugu yake Esau kwa miaka mingi, lakini siku alipotambua kuwa Lipo jeshi la pili pamoja naye (Mahanaimu)..alisonga mbele kwa ujasiri na Bwana akampatanisha na Adui yake, Yule Yule adui yake akageuka kuwa kipenzi chake.. Vile vile yale majeshi yaliyotumwa kumkamata Elisha na Mtumishi wake, yaligeuka kuwa marafiki wa Elisha..(kwani baada ya lile tukio hayakurudi tena Israeli kwa kipindi kirefu sana 2Wafalme 6:23).

Na wewe kama umeokoka, songa mbele usikwamishwe na vitisho vya shetani, kwasababu walio upande wako ni wengi kuliko walio upande wa adui.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

BWANA AWEZA KUKUPA ZAIDI SANA KULIKO HIZO.

SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?

Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?

KWANINI UPIGE MISHALE CHINI?

MJUMBE ASIYEKUWA NA UJUMBE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ezra ndambuki / from Kenya
Ezra ndambuki / from Kenya
10 months ago

Kwa hakika hayo yote ni Amina na KWELI
Mwanadamu anaweza kuona amefika mwisho Lakini kwa mungu bado
Nilikua naona nimefika mwisho kwa vitisho vya shetani Lakini mungu akaniokoa haleluya