KWANINI UPIGE MISHALE CHINI?

KWANINI UPIGE MISHALE CHINI?

Ahimidiwe Bwana wetu Yesu Kristo, utukufu na heshima vina yeye milele na milele.Amen

Wakati fulani mfalme wa Israeli aliyeitwa Yehoashi alimfuata Elisha ili kumjulia hali kabla hajafa.

Kama tunavyosoma habari ile  Elisha alimwambia achukue mshale kisha aurushe upande wa mashariki kupitia dirishani. Na alipofanya vile Elisha alimwambia huo ni mshale wa ushindi dhidi ya maadui zake washami..

Hivyo mfalme alipoona vile jinsi alivyopewa maagizo mepesi na yenye uhalisia wa ushindi  kwa tendo la kutupa mishale, hakuwa na shaka yoyote kusikia pengine Elisha atampa maagizo mengine kama hayo, ya kurusha mishale mingine mingi Zaidi ili kuwapiga maadui zake walio karibu naye.

Lakini mambo yalikuwa ni kinyume na mtazamo wake kwani Elisha alimwagiza apige mishale yake ardhini badala ya kuirusha juu, kama alivyofanya hapo kwanza, tendo hilo  likaweka ukakasi kwake “kutupa mishale ardhini”!? pengine alidhani ni mishale inayomrudia yeye.

Tusome..

2 Wafalme 13:14-19

[14]Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!

[15]Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale.

[16]Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.

[17]Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.

[18]Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha.

[19]Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.

Umeona, hakujua kuwa ile ya kupiga chini ndio mishale ya ushindi, kinyume chake akawa na hofu matokeo yake akapiga michache tu (yaani mitatu)..

Ni jambo la kawaida hata leo, Mungu anawaagiza watakatifu wake warushe mishale mingi mahali ambapo ni  kinyume na matarajio yao..lakini mashaka yanawaingia, wanaona kama wanafanyakazi bure, na kupoteza nguvu.

Ndugu yangu vita vya kiroho  ukivitazama kwa jicho la mwilini ni rahisi sana kukata tamaa, kwasababu unaweza ukajiona kama unapoteza tu nguvu zako na muda..kama vile kupiga mishale chini..

Unapokuwa katika maombi, usitazamie kuona badiliko lolote la nje labda  mbingu imekuwa  ya blue, au usikie mapanga yakipigwa na malaika katika anga la kwanza hapana..zaidi sana utaona  ni kama siku nyingine tu ya kawaida, umeomba bure, umeuchosha mwili bure. Lakini katika roho umeangusha ngome nyingi sana za ibilisi, tena na kwa jinsi unavyozidi kudumu zaidi na zaidi katika kuomba ndivyo unavyomfukuza shetani mbali nawe kabisa kabisa .

Hivyo hupaswi kukata tamaa au kuacha kuomba kwasababu hiyo mishale ya ardhini ndio yenye mapigo ya Mungu kuliko ile ya juu.

Unaposhea Neno la Mungu na wengine mtandaoni unaweza usione Matokeo yoyote ya kile unachokifanya, lakini wewe endelea Shea sana kwasababu hiyo ndio mishale ya ushindi unayoidharau wewe.

Unapohubiri mitaani au masokoni, unaweza ukaona kama unawapigia tu watu makelele, au watu hawakusikilizi, lakini hiyo ndio mishale ya ushindi katika vita vyako.

Njia za Mungu sio njia zetu. Wewe utarusha juu, yeye atataka urushe chini..huwezi kumpangia kanuni ya vita.

Hivyo tufanyapo jambo lolote la ki-Mungu tusipime-pime sana au kuchunguza-chunguza sana kwa jicho la nje, kwasababu ukifanya hivyo itakuwa ni rahisi kukata tamaa…bali tufanye kile alichotuagiza kwa bidii kana kwamba tunapoteza nguvu zetu bure, na matokeo yake tutakuja kuyaona baadaye katika ulimwengu wa roho.

Ongeza michale yako ya chini.

Bwana akubariki.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?

Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?

Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?

Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?

Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments