Kitambi kilichopo kwenye Ini ndio kilikuwaje?

Kitambi kilichopo kwenye Ini ndio kilikuwaje?

Jibu: Tusome,

Walawi 3:3 “Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,

4 na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa”.

Kulingana na lugha yetu, tumezoea kutafsiri neno “kitambi” kama “tumbo lililotoka nje”..yaani unapotaja kitambi tu!, basi picha ya kwanza kujitengeneza akilini ni “mtu mwenye tumbo kubwa” lakini kiuhalisia neno kitambi tafsiri yake sio tumbo.. bali ni “kitu chochote ambacho kimevimba au kimejaa na kutengeneza mduara”. Pulizo lililojaa upepo au lililojaa maji limetengeneza kitambi! Kwa ule ujazo na ule mduara.

Kadhalika “Ini” linacho “kitambi” na kitambi chenyewe ndio ule mduara wake.. Na ini linatabia ya kuongezeka ukubwa na kupungua kama vile tumbo lilivyo, mtu leo utamwona yupo kawaida kesho atakuwa na kitambi, kadhalika wachunguzi wanasema Ini nayo linakua, hata likipunguzwa baada ya kipindi Fulani linaota tena na kuwa kubwa, (kitambi chake kinaongezeka..)

Bwana alimwagiza Haruni na wanawe kulitwaa Ini, Pamoja na kitambi chake hicho, Pamoja na figo na mafuta yaliyo yaliyoshikamana na viungo hivyo, na kuviteketeza juu ya madhahabu kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana.(Maagizo hayo Bwana aliwapa wakati watu watakapotaka kuleta sadaka za amani mbele za Bwana)

Na kwanini Bwana alivihitaji viungo hivyo vya ndani vichache tu! na si viungo vyote kama miguu, nyama n.k? bali alihitaji tu FIGO na INI?

Ni kwasababu viungo hivyo viwili yaani FIGO, Pamoja na INI vinahusika katika kuchuja sumu inayoingia Mwilini. Mtu au Mnyama akiondolewa FIGO au INI anamuda mfupi sana wa kuishi, kwani atakufa kwa sumu itakayoingia mwilini mwake kwa njia ya chakula au maji!..kwani vyakula tunavyokula vinayo sumu nyingi lakini ini, inavunja vunja ile sumu ya kukibakisha kile chakula salama.

Ikifunua kuwa na sisi tunapomtolea Mungu sadaka za amani kama hizo, basi sehemu ya roho zetu inayohusika na upambanuzi wa roho za uadui, Bwana anaziongoza yeye, tunajikuta tunakuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua mabaya na kuyashinda, kadhalika mambo yote mabaya ambayo ni sumu kwetu, tunakuwa tunauwezo wa kuyapambanua.. kama vile Figo na Ini zilivyokuwa na uwezo huo.

Hivyo kuna umuhimu pia mkubwa sana wa kumtolea Bwana, hususani tunapomtolea kwa hiari na si kwa kulazimishwa, kuna baraka nyingi sana za kiroho.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?

UTAWALA WA MIAKA 1000.

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?

Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments