Jibu: Tiro na Sidoni ni miji iliyokuwa katika nchi inayoitwa LEBANONI. Tofauti na nchi nyingine ambazo zilibadilika majina baada ya miaka mingi kupita, lakini nchi ya Lebanoni, imeitwa kwa jina hilo hilo tangu nyakati za biblia hata leo.
Tiro na Sidoni ni miji ambayo ipo karibu karibu, (Kusini Mashariki mwa Nchi ya Lebanoni), na miji hii enzi za biblia ilikuwa ni miji ya kibiashara, lakini iliyojaa machukizo mengi.
Kwasasa nchi ya Lebanoni ina miji mikubwa minne, Ambayo ni Beiruti, Tripoli, Sidoni na Tiro. Mji wa Sidoni ni mkubwa kuliko Tiro na katika Lebanoni ndiko ulipokuwepo pia Mji wa Tarshishi, ule ambao Yona aliukimbilia ili apate kujiepusha na uso wa Bwana.
Kwasasa nchi hii ya Lebanoni inakaliwa na Waarabu, na ni nchi ambayo ipo katika upande wa Kaskazini mwa Israeli, Eneo kubwa la Nchi ya Lebanoni, ni misitu na ndio huko Mfalme Sulemani alipotolea Miti aina ya Mierezi kwaajili ya ujenzi wa Hekalu la Mungu.
Nchi ya Lebanoni kwasasa ina uadui mkubwa sana na Nchi ya Israeli. Na unabii unaonyesha katika Ezekieli 38 na 39 kuwa siku za mwisho Lebanoni pamoja na nchi za kando kando zitashirikiana na Nchi ya Urusi kwa lengo la kuifuta Israeli katika uso wa dunia, lakini zitapigwa zote, kwasababu Mungu wakati huo atasimama upande wa watu wake Israeli.
Kwaufupi miji ya Tiro na Sidoni imebeba ufunuo mkubwa katika matukio ndani ya biblia. Kasome Mathayo 11:21-22, Yoeli 3:4, Zekaria 9:1-4, na Matendo 12:20
Lakini lililo kubwa zaidi ni ufunuo mji huo uliobeba, kumhusu shetani.. Biblia inamtaja mkuu wa Mji wa Tiro katika ulimwengu wa roho, kwamba ni shetani mwenyewe.
Ezekieli 28:1 “Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu……
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.
14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.
15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”.
Na shetani si mkuu tu wa Tiro, bali biblia imezidi kutupa mwangaza kuwa ni mungu wa ulimwengu mzima (2Wakorintho 4:4).. Yaani mifumo yote ya kishetani iliyopo duniani ni yeye muasisi.
Je umempokea Yesu?
Kumbuka hizi ni siku za mwisho na Kristo yupo Mlangoni.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
Mada Nyinginezo:
Kwanini Herode aliwakasirikia watu wa Tiro na Sidoni? (Matendo 12:20)
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
About the author