Mathayo 6:30 “Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?”
Neno hili “kalibu” limerudiwa pia kutajwa katika Luka 12:28, na maana ya neno hili ni “TANURU LA MOTO”. Kwa kawaida baada ya kusafisha mazingira, kwa kuondoa Nyasi au takataka huwa zinatupwa katika tanuru la moto, sasa tanuru hilo ndilo linaloitwa “Kalibu”, Na Bwana Yesu alitoa mfano huo kuonyesha maisha yetu jinsi yalivyo na thamani mara nyingi zaidi kuliko maua ya kondeni.
Kwani kama Mungu anavyoyavika utukufu maua ya kondeni, kwa rangi rangi zake za kuvutia, basi sisi ni zaidi sana mbele zake kuliko hayo MAUA ya kondeni, ambayo leo yapo lakini kesho yanatupwa motoni.. Sisi tuna thamani mbele zake kuliko maua, maana yake sisi atatuvisha zaidi kuliko Maua, atatulisha zaidi kuliko ndege, atatubariki kuliko viumbe vyote vya asili. Huo ni upendeleo wa kipekee sana.
Tunachopaswa kufanya ni kuutafuta tu ufalme wake na haki yake, halafu hayo mengine ya chakula, mavazi tumwachie yeye, kasema atatuzidishia, na yeye kamwe hawezi kusema uongo.
Luka 12:29 “Ninyi msitafute mtakavyokula wala mtakavyokunywa; wala msifanye wasiwasi,
30 kwa maana, hayo yote ndiyo watafutayo mataifa ya duniani, lakini Baba yenu anajua ya kuwa mna haja na hayo.
31 Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa.
32 Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme”
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je suruali ni vazi la kiume tu?
Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?
About the author