Jibu: Tusome,
Yohana 5:37 “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. SAUTI YAKE HAMKUISIKIA WAKATI WO WOTE, WALA SURA YAKE HAMKUIONA. 38 Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.”
Yohana 5:37 “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. SAUTI YAKE HAMKUISIKIA WAKATI WO WOTE, WALA SURA YAKE HAMKUIONA.
38 Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.”
Hapa Bwana Yesu hamaanishi kwa Wayahudi hawajawahi kuisikia sauti ya Mungu, wala kuliona umbile lake!. Hapana bali andiko hilo linamaansha kuwa Mungu alijidhihirisha kwao kimaumbile lakini hawakumwona na vile vile alijidhihirisha kwao kisauti lakini hawakumsikia.
Sawasawa kabisa na alivyosema katika Kitabu cha Isaya
Isaya 50:2 “Basi, NILIPOKUJA, MBONA HAPAKUWA NA MTU? NILIPOITA, MBONA HAPAKUWA NA MTU ALIYENIJIBU? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu”.
Umeona hapo?.. kumbe kuna wakati Bwana anatujia kimaumbile lakini hatumwoni?… Sasa utauliza ni wakati gani anatujia hatumwoni, na ni wakati gani anapaza sauti yake hatuisikii??
Kupitia watumishi wake wa kweli, wanapotujia kama wageni na kutuletea habari njema, ujio wao unafananishwa kabisa na ujio wa Kristo kwetu kimaumbile, haihitaji yeye Mungu atutokee ndio ihesabike kuwa tumeliona umbile lake, bali watumishi wake tu kutujia tayari hao ni umbile lake…… utasema hilo tunalithibitisha vipi kimaandiko??
Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, KADIRI MSIVYOMTENDEA MMOJAWAPO WA HAO WALIO WADOGO, HAMKUNITENDEA MIMI. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, KADIRI MSIVYOMTENDEA MMOJAWAPO WA HAO WALIO WADOGO, HAMKUNITENDEA MIMI.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Umeona?.. Vile vile tusiposikiliza sauti za watumishi wake, ni sawa na hatujaisikiliza sauti yake!.. Ndio maana hapo katika Isaya 52:2 anasema “nilipoita mbona hamkuitika?”.. maana yake ni kwamba wenyewe walidhani sauti wanayoisikia ni ya mwanadamu kumbe ni ya Mungu.. vile vile walidhani umbile walionalo mbele yao ni la mwanadamu kumbe ndio umbile la Mungu, kwahiyo wakayadharau maneno ya Mungu aliyoyazungumza kupitia watumishi wake..
Na hapa Kristo anarudia tena maneno hayo hayo ya Isaya na kusema… “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. SAUTI YAKE HAMKUISIKIA WAKATI WO WOTE, WALA SURA YAKE HAMKUIONA.”.. Maana yake Mungu alizungumza nao mara nyingi, na kuonekana kwao mara nyingi lakini hawakuwahi kumsikia wala kumwelewa wala kumfahamu hata mara moja, kwasababu mioyo yao ilikuwa mbali naye.
Na sisi tunajifunza kuwa sauti ya Mungu haiji kwetu kama sisi tunavyotaka au tunavyopanga, wala Mungu hatujii kimaumbile kama sisi tunavyotaka!..
Ni wengi sana wanafunga na kukesha ili kwamba Mungu awatokee, na waisikie sauti ya Mungu kama vile redio,..kama unafanya hivyo nataka nikuambie kuwa “unapoteza muda wako”.. kwasababu hiyo sio Njia ya MUNGU kuzungumza na sisi, hizo ni njia zetu sisi wanadamu za kuwasiliana..Mungu yeye anazo njia zake, ni lazima tuzijue hizo, tusilazimishe atumie zetu… “atafanya hivyo akipenda”, lakini si kanuni yake!.
Ukitaka kuisikia sauti ya Mungu vizuri, soma Neno na kulitafakari, Sikiliza mahubiri ya watumishi wa Mungu wa kweli, na ishi maisha matakatifu. Hapo utamwona Mungu sana katika maisha yako na utamsikia sana.
Bwana atusaidie na kutubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.
Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?
FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.
Rudi nyumbani
Print this post