Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Huu ni mfululizo wa masomo maalumu kwa ajili ya wanawake: Ikiwa hukupata chambuzi nyingine za nyuma basi fungua link hii  uweze kuzipitia >>>   MAFUNDISHO KWA WANAWAKE

Mwanzo 34:1-3 Inasema..

“Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, AKATOKA KUWAONA BINTI ZA NCHI.  2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.  3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri”

Dina alikuwa ni binti wa Yakobo, aliyejitunza na kujiheshimu, alikaa chini ya Mama zake akifundishwa desturi za uzao wa Ibrahimu unavyopaswa uwe. Akafahamu kuwa uzao wao haupaswi kuchanganywa na uzao wa ukoo mwingine, Ili Baraka ya Ibrahimu aliyoahidiwa kwa uzao wake isiingiliwe na doa.

Lakini Tunaona, jambo moja alilolifanya Dina, ambalo pengine hakujua mwisho wake utampelekea pabaya. Na jambo lenyewe “ni yeye kutoka na kwenda kuonana na mabinti wa nchi”. Kama msichana alipoona mabinti wa mataifa mengine, wanaishi maisha ya kidunia, maisha ya anasa, maisha ya ukisasa. Na yeye naye akatamani kwenda kuunga urafiki nao, bila kujua mwisho wake utakuwaje.

Hivyo kidogo kidogo, akaanza kuchukuliwa na desturi za wanawake wa kidunia, akaanza kujichanganya, siku ya kwanza, siku ya pili, wiki ya kwanza wiki ya pili, mwezi wa kwanza, mwezi wa pili. Kidogo kidogo wale mabinti wa kidunia waanza kumfundisha tabia mbaya..Pengine wakaanza kumwambia “Mbona wewe ni mrembo, hadi sasa huna boyfriend”..Mbona una shepu zuri, embu vaa hizi nguo fupi uonekane na wanaume..Embu twende leo disco, tukakutane na vijana wenzetu, tule maisha, ujana maji ya moto..

Akawa anawasikiliza, na huko ndipo akakutana na huyo Shekemu, akamlaghai, kisha akambikiri..Taarifa zikawafikia ndugu zake, wakakasirika sana Simeoni na Lawi, hadi kufikia kitendo cha kwenda kuwaua watu wote wa huo ukoo. Kwasababu waliona tendo alilofanya Dina, ni chukizo kubwa sana kwa jamii yao. Kuuchafua uzao uliobarikiwa, kuvunja maagano ya Mungu.

Nini Bwana anataka mabinti na wanawake wajifunze?

Kabla ya kuanguka katika dhambi, ushawihi huwa unaanza kwanza kwa marafiki wanaokuzunguka.  Angalia ni watu wa namna gani uliozoena nao, au uliounga urafiki nao, au unaokaa nao muda mrefu. Mabinti wengi waliookoka, hawajafundishwa kuvaa vibaya na wanaume wazinzi, bali na mabinti wenzao, hawajafundishwa kwenda disco au kunywa pombe na wanaume, bali mabinti wenzao. Hawajafundishwa kwenda kwa waganga na kaka zao, bali wanawake wenzao, hawajafundishwa kusengenya na jamii, bali ni wanawake wenzao wanaokutana nao masaluni na mabarazani.

Hawa ndio maadui wa kwanza. Dina hakutoka kwenda kumtafuta Shekemu, alitoka kuwatazama mabinti  tu wa kidunia na huko huko wakamuunganishia Shekemu. Laiti angetulia nyumbani akakaa na wale wabinti wenzake wa ukoo mmoja hata kama ni washamba, angekuwa salama.

Wewe kama mwanamke usipende kuunga urafiki na wanawake ambao hawajaokoka, ambao hawana habari na Mambo ya ufalme wa mbinguni, upo chuo, upo shuleni, upo kazini, ni heri ubaki kivyako vyako, kuliko kujiingiza hatarini. Siku zote uangamivu unavyokuja huwa unaanzia mbali sana, hivyo kuwa makini, tafuta watu waliodhamiria kuishi maisha matakatifu, hao ndio wawe marafiki zako wa karibu, washauri wako, uige tabia zao, kataa kampani za kipepo, acha wakuone mshamba, lakini roho yako ipo salama, acha upitwe na fashion, acha upitwe na uzuri lakini jina lako lipo katika kitabu cha uzima.

Majira tunayoishi ni ya kung’ang’ania kwa nguvu wokovu tuliopewa, ni kuwa siriazi kweli kweli, kwasababu maelfu kwa maelfu ya watu wanaangamia, wanashindwa kumaliza mwendo wao salama hapa duniani wanaponzwa na marafiki, Unadhani na sisi tukiwa walegevu, tunadhiria kila kitu tu kinachokuja mbele yetu, tutawezaje kupona. Njia imesonga, mlango ni mwembamba, tunajiingiza kwa nguvu, isitoshe muda tuliobakiwa nao ni mchache. Hivyo hatupaswi kuwapa nafasi watu wakidunia katika maisha yetu.

Tujifunze kwa Dina. Tuwe salama. Kataa, kampani za kipepo!

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

MAFUNDISHO KWA WANAWAKE

FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!

MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.

Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?

Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Eliabu
Eliabu
5 months ago

Je kwann vijana hatuaminiki kwenye nyumba za ibada

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Amina kwa Wanawake waliokolewa na Yesu. Muishi Maisha kwa kiasi maana wateule wa Mungu wana njia yao ya kupitia ambayo watu wengi wa kidunia wanaipinga na hawaitakii.