Kwanini Yuda aliitwa Iskariote?..nini maana ya Iskariote?

Kwanini Yuda aliitwa Iskariote?..nini maana ya Iskariote?


Jibu: Iskariote sio jina la mtu fulani, au la mzazi wa Yuda, bali ni jina lenye maana ya “Mtu wa Keriothi/ Kariote”…

Neno Iskariote ni neno la kigiriki lililoungwa na maneno mawili: “Is” ambalo maana yake ni “mwana wa” na la pili ni “Kariote”..likimaanisha mji wa Kariote au Keriothi
Kwahiyo ukiunganisha maneno hayo mawili maana yake ni “Mwana wa Keriothi”

Na Keriothi ni mji uliokuwepo katika Nchi la Moabu, ambayo kwasasa ni maeneo ya nchi ya Jordani.
Na Wamaobu walikuwa ni watu wa mataifa, hawakuwa waIsraeli, kwa urefu kuhusu Taifa hili unaweza kufungua hapa >>> MOABU NI WAPI

Sasa swali ni je! Kwanini Yuda aitwe hivyo, na asiitwe tu Yuda! Kwanini atambulike kama Mwana wa Keriothi(Iskariote)?… kulikuwa na umuhimu gani yeye kutajwa kwa jina hilo?.

Jibu rahisi ni kwamba, alitajwa vile ili kumtofautisha na wakina Yuda wengine, kwasababu kulikuwa na watu wengi wanaoitwa Yuda ambao pia walikuwa wanafuatana na Yesu. Na Kuna mwingine alikuwa mdogo wake Yesu.

Kwa mfano utaona kuna wanafunzi wawili wa Bwana Yesu waliokuwa na majina yanayofanana..wote walikuwa wanaitwa Simoni, sasa ili kuwatofautisha ndio mmoja akajulikana kama Simoni Petro na mwingine Simoni Mkananayo. (Mathayo 10:2-4).

Vile vile kulikuwa na wanawake wengi waliomfuata Bwana walioitwa Mariamu, sasa ili kuwatofautisha hao akina Mariamu, ndipo hapo wengine wakatajwa kulingana na miji waliyotokea mfano Mariamu aliyetolewa pepo saba alijulikana kama Mariamu Magdalene, kufuatia mji aliotokea ujulikanao kama Magdalene. (Luka 8:2).

Na Yuda Iskariote aliitwa hivyo kufiatia mji ambao Baba yake alitokea (Keriothi).

Yohana 6:71 “Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara”.

Soma pia Yohana 13:2, na Yohana 13:26, huenda baba yake Yuda alikuwa ni myahudi lakini mwenyeji wa Kerioth pamoja na Yuda mwanae.

Kuhusiana na mji wa Keriothi au Kariote, pitia mistari ifuatayo; Amosi 2:2, Yeremia 48:24, na Yoshua 15:25.

Na sisi Bwana anatujua majina yetu kulingana na tabia zetu.

Kutoka 33:17 “BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako”

Mbele za Mungu kila mtu anajulikana kwa tabia yake…fulani mcha Mungu, fulani mwombaji, fulani mkaribishaji, fulani mwizi, fulani mzinzi, fulani msengenyaji.

Bwana atujalie tujulikane kwa majina mazuri na mema mbele zake ili tupate neema.

Kutoka 33:17 “BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako”

Maran atha

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.

ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.

JINA LA MUNGU NI LIPI?

TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Silvest nipo mpanda tz
Silvest nipo mpanda tz
1 year ago

Asante mtumishi

Anonymous
Anonymous
1 year ago

Nashukuru, kazi njema Mungu azidi kuwa jaliya Neema Na bidii , ,,, ningependa Sana masomo kuhuzu Kita u cha ufunuo nijuwe umuhimu wake siku Ile mwana wa Mungu anakuja , Ufunuo 13: 1 kuhuzu naomba ,666
Ufunuo 18: Kwa jumla ,,
Fred lusweti ,,, Nairobi