Beelzebuli ni nani? (Mathayo 12:24).

Beelzebuli ni nani? (Mathayo 12:24).

Swali: Katika biblia Beelzebuli alikuwa ni nani?, na kwanini Mafarisayo wamwite Bwana Yesu Belzebuli/.

Jibu: Jina Beelzebuli ni mwunganiko wa maneno matatu (3), Beel-ze-buli.. “Beel” maana yake ni
“bwana au mkuu”“Ze”  ni kiunganishi chenye maana ya “wa”  na “Buli” ni pepo wachafu mfano wa inzi.

Kwahiyo ukiunganisha maneno hayo  matatu linakuja neno  “Mkuu/bwana wa pepo”.. sawasawa na biblia ilivyotafsiri katika Mathayo 12:24.

Mathayo 12:22  “Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona.

23  Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi?

24  Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa BEELZEBULI MKUU WA PEPO”.

Sasa huyu Beelzebuli mkuu wa pepo ni nani?

Si mwingine Zaidi ya “shetani mwenyewe”. Biblia inamtaja shetani kuwa ndiye mkuu wa ufalme wa giza, na ndiye mkuu wa pepo wote walioasi (Ufunuo 12:9).

Kwahiyo Mafarisayo walipoona Bwana anatoa mapepo kwa uweza wa Mungu na wenyewe hawawezi, wakaingiwa na wivu, na kuamua kuzusha kuwa anatoa pepo kwa uwezo wa shetani (beelzebuli) na si kwa uwezo wa kiMungu. Lakini jibu la Bwana lilikuwa “shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake, vinginevyo ufalme wake hautasimama”.

Mathayo 12:26 “NA SHETANI AKIMTOA SHETANI, AMEFITINIKA JUU YA NAFSI YAKE; BASI UFALME WAKE UTASIMAMAJE?

27  Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu.

28  Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajili”

Hii ikifundisha kuwa uweza wa Mungu pekee ndio unaoweza kutoa pepo!. Shetani kwamwe hawezi kutoa pepo kwani mapepo yake yote yanafanya kazi yake..anachokifanya ni kubadilisha tu tatizo ndani ya mtu, au kuongeza tatizo ndani ya mtu.

Watu wanaoenda kwa waganga na kusema wameaguliwa na kupona, kiuhalisia hawajapona bali wamebadilishiwa tatizo au wameongezewa pepo lingine juu ya lile lililokuwepo ili kutuliza tu maumivu, lakini baada ya muda lile tatizo litajirudia na lingine kubwa Zaidi ya hilo (kwasababu kamwe shetani hawezi kulitoa pepo lake ndani ya mtu, kwasababu yeye ndiye kaliweka humo, sasa akilitoa si atakuwa anafanya kazi ya Mungu, na yeye kamwe hawezi kufanya hivyo, kwasababu hana mapenzi na wanadamu, yeye anachokitafuta ni kuwaangamiza wadamu na si kuwaweka huru).

Kwahiyo wanaoenda kwa waganga ili kupata tiba, hakuna tiba yoyote wanayoipata Zaidi ya kuongeza matatizo..Suluhisho la tabu na matatizo yote ni Yesu tu!, huyo ndiye maandiko yanasema kuwa akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli (Yohana 8:36), na si waganga wala wachawi wala watabiri.

Kama umewaza kwenda kwa waganga kwasababu ya tatizo ulilokuwa nalo, leo hii badilisha fikra zako, kule unaenda kuongeza matatizo na si kupunguza. Mkimbilie Yesu, huyo peke yake ndiye Suluhisho na ndiye mwenye upendo wa kweli.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.

Je ni kweli hakuna aliyepaa mbinguni zaidi ya Mwana wa Adamu? (Yohana 3:13)

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments