Miimo ni nini na kizingiti ni nini?

Miimo ni nini na kizingiti ni nini?

Katika biblia Miimo ni nini na kizingiti ni nini?

Jibu: Miimo ni nguzo mbili za mlango zinazosimama upande wa kuume na wa kushoto mwa mlango.

Mfano wa hiyo ni ile Samsoni aliyoing’oa ya geti la wafilisti

Waamuzi 16:3 “Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, NA MIIMO YAKE MIWILI, akaing’oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni”.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu Miimo katika mistari ifuatayo Kumbukumbu 6:9, 1Wafalme 6:33, na Isaya 57:8.

Na kizingiti ni nguzo moja ya mlango inayolala ambayo inakuwa upande wa juu wa mlango (wakati mwingine pia inawekwa upande wa chini wa mlango) Kwamfano utaona wakati wana wa Israeli wanatolewa Misri, waliambiwa wapake ile damu ya mwanakondoo kwenye vizingiti vya nyumba na  kwenye miimo yake, ili yule Malaika alitumwa kuharibu asiingie na kuua wazaliwa wa kwanza wa nyumba hizo.

Kutoka 12:7 “Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na KATIKA KIZINGITI cha juu, katika zile nyumba watakazomla”.

Miimo na vizingiti vinaweza kuwa vya malighafi yoyote, aidha mbao, chuma, udongo au shaba.

Unaweza kusoma zaidi juu ya kizingiti/vizingiti katika mistari ifuatayo Ezekieli 10:4, 1Wafalme 6:31, na 1Wafalme 14:17.

Lakini Miimo na vizingiti vinafunua nini kiroho?

Maandiko yanasema Miili yetu ni Nyumba (Hekalu la Roho Mtakatifu) 1Wakorintho 6:19 na 1Wakorintho 3:16 na Kama ni Nyumba ya Roho Mtakatifu basi ni lazima ina Mlango, na kama ina mlango ni lazima ina miimo na vizingiti.

Sasa Mlango wa Hekalu la Roho Mtakatifu ni mioyo yetu..

Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”

Na kama mioyo yetu ni Malango basi ni lazima ina Miimo yake na Vizingiti vyake.. na hivyo si vingine zaidi ya Macho yetu na Masikio masikio yetu. Masikio ni vizingiti na macho ni miimo.

Mioyo yetu inapokea vile tunavyovisikia na na macho yetu vile tunavayoviona. Hivyo kama macho yetu yametakaswa kwa damu ya Yesu Kristo katika ulimwengu wa roho na masikio yetu yametakaswa kwa damu ya Yesu Kristo basi hapo ni sawa na ile nyumba iliyopakwa damu ya mwana kondoo katika miimo ya milango yake na vizingiti vyake nyakati za Israeli kutoka Misri, Na hivyo uharibifu utakapofika hautatukuta.

 Lakini kinyume chake kama Macho yetu ni ya uasi na masikio yetu ni ya ukaidi basi hata mioyo yetu itakuwa michafu na hivyo tutalinajisi Hekalu zima la Mungu ambalo ndio miili yetu na hivyo kujiweka katika hatari ya kuharibiwa sawasawa na maandiko yanavyosema.

1Wakorintho 3:17 “Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”

Je umeokoka?, je umetakaswa kwa damu ya Yesu?.. Kama bado unasubiri nini?, mpokee Yesu leo kwa kutubu na kubatizwa na kujazwa Roho Mtakatifu.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma? 

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments