SWALI: Nini maana ya Zaburi 125:3 “ Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki; Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu”.
JIBU: Mstari huo unatuonyesha jinsi Mungu anavyowatenga watu wake na adhabu ambazo zinawahusu waovu. Kwamba kamwe fimbo ya adhabu haiwezi kuwahusu watu wa Mungu, Ndio maana ya hilo neno ‘Kwa maana fimbo ya udhalimu Haitakaa juu ya fungu la wenye haki;.. Ni mfano tu wa wana wa Israeli wakati ule walipokuwa Misri, Mungu aliwatenga na wamisri na kuwaweka kule Gosheni, na mpigo yote yalipokuja hayakuwakuta wana wa Israeli, bali wamisri tu. Hata baadaye alipotaka kuliadhibu taifa zima, bado aliwaficha watu wake ndani ya nyumba, na Yule malaika aliyeshushwa kuwauwa watu, hakupita katika nyumba zao. Kuonyesha kuwa fimbo za makosa Mungu hana desturi ya kuzijumuisha na watu wake, isipokuwa tu wamekataa wenyewe. Ndivyo ilivyokuwa kwa Nuhu, na Lutu.
Na anafanya hivyo kwasababu gani? Ndio hapo anasema ili “Wenye haki wasije wakainyosha Mikono yao kwenye upotovu”. Kwamba anawataadharisha watu wake wasidiriki kufanya makosa kama hayo hayo ya waovu kwasababu na wenyewe adhabu inaweza kuwakuta vilevile. Na kweli ndivyo ilivyokuwa kwa wana wa Israeli baadaye, walimwacha Mungu wakaanza kuitumikia miungu, na matokeo yake Mungu akawarudisha tena utumwani, na miji yao kubomolewa.
Hivyo, ni kutuonya kuwa sisi tuliokoka, kamwe tusijichanganye na maovu kwasababu adhabu ya makosa yaweza kutupata na sisi pia, kwasababu Mungu hatazami uso wa mwanadamu, bali ulekevu wako kwake.
Shalom.
Kwa maana nyingine ya mistari mbalimbali ya biblia tembelea website yetu hii >>> www.wingulamashahidi.org.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kulabu ni nini katika biblia?(2Wafalme 19:27)
Miimo ni nini na kizingiti ni nini?
Tirshatha ni nini? (Ezra 2:63)
Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
Je Bwana Yesu aliruhusu wanafunzi wake kubeba Fimbo au hakuwaruhusu? (Marko 6:8 na Mathayo 10:10).
Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?
UTARATIBU WA KUTOA FUNGU LA 10 UPOJE?.
Rudi nyumbani
Print this post