Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.

SWALI: Biblia inamaana gani kusema Yesu atawachunga kwa fimbo ya chuma..kwanini iwe ya chuma?

 Ufunuo wa Yohana 19:15
[15]Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

JIBU: Fimbo ya mchungaji sikuzote ni fimbo ya mti…ambayo ukichapwa haiwezi kukuletea madhara makubwa sana, zaidi ya maumivu tu mwilini..

Lakini tengeneza picha unapigwa kwa chuma iliyoundwa kwa mfumo wa fimbo..kama vile nondo ngumu..unategemea ni nini kitatokea hapo katika mwili? Sio kusikia tu maumivu lakini pia kuharibika kwa baadhi ya viungo kama vile misuli na mifupa kuvinjika kutatokea. Na kama ukipigwa sehemu mbaya kama vile kichwani..moja kwa moja ni mauti. Kwasababu anayekupiga hana lengo la kukuadhibu bali kukuharibu.

Ndivyo inavyomuonyesha Bwana Yesu, atakapokuja kuwa katika ule utawala wa miaka 1000 hapa duniani.

Kama vile tunavyosoma katika maandiko kuwa yeye ni mchungaji mwema (Yohana 10:14-16)..Ikiwa anamaanisha kuwa Leo hii anatuchunga kondoo wake kwa fimbo ya mti, na ndio maana anapotuadhibu hatuangamii kabisa kwasababu sisi ni kondoo anayetupenda na kututakia mema, anafanya hivyo kwa lengo la kitufanya tu tusitoke katika njia adui akatuangamiza.

Lakini atakapokuja na kutawala kama mfalme wa wafalme biblia inatuambia Amani itatawala duniani kote…kiasi kwamba waovu watakuwepo lakini kwa ule utiisho wake tu, hakuna dhambi yoyote itakayochukua nafasi, kwani adhabu zitakuwa kali kwa watu watakaojaribu kuipindisha amani.

Kwasababu wakati huo atakuwa hachungi kondoo tena kwasababu watakuwa wameshaokolewa, bali atashughulika na mbwa mwitu, hao ndio watapigwa kwa fimbo hiyo kali.

Isaya 65:20
[20]Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.

Hiyo ndio fimbo ya chuma..uovu wala waovu hawatavumilika kwa namna yoyote ile..Vilevile kushindwa kutekeleza maagizo ya ufalme wa Bwana Yesu utakumbana tu na fimbo hiyo ya chuma. Soma (Zekaria 14:17-20).

Kumbuka Jambo hilo atalitekeleza Kristo pamoja na watakatifu wake, wale ambao waliushinda huu ulimwengu wakaenda naye katika unyakuo.

Ufunuo wa Yohana 2:26-27
[26]Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
[27]naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.

Hivyo ni vizuri ukafahamu kuwa Kristo anazo fimbo mbili…Ni heri sasa ukubali kuchungwa naye kwa fimbo ya miti…wakati utafika kabla hata ya utawala wenyewe kuanza…fimbo hiyo ya chuma ataipitisha kwa ulimwengu mzima, kwa yale mapigo atakayoyashusha humu ulimwengu ili kuwaangamiza wote..

Si jambo la kulitamani hata kidogo. Ni heri umpe Kristo maisha yako leo hii ayaokoe, akupe uzima wa milele. Hizi ni nyakati za mwisho. Unyakuo upo mlangoni.

Bwana akubariki.

Ikiwa utapenda kupata somo lote la utawala wa miaka 1000 wa Yesu Kristo utakavyokuwa..nitumie ujumbe inbox kwa namba hii +255693036618..nikupe somo lake.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?

Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?

Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
2 years ago

Amen.

Javan Chihimba
Javan Chihimba
2 years ago

Asante sana.