Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili?

Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili?

SWALI: Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili, na kumfedhehi kwa dhahiri?

JIBU: Neno hilo tunalisoma katika kifungu hiki;

Waebrania 6:4  Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5  na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,

6  wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.

Anazungumzia kundi la watu ambao walishapitishwa katika hatua zote tano (5), za uzuri wa Mungu na matendo makuu ya Mungu ndani ya maisha ya mwaminio. yaani.

i)Kupewa nuru ya injili,

ii)kuonja kipawa cha mbinguni,

iii) kufanywa mshirika wa Roho Mtakatifu,

iv) kulionja Neno zuri la Mungu,

v) na kuonja nguvu za zamani zijazo.

Kwamba watu wa namna hii wakianguka, kamwe haiwezekani kuwafanya wakatubu upya.

Lakini halengi kundi la watu walio wachanga kiroho, au waliorudi nyuma kwa kukosa maarifa, au kudanganywa au kwasababu nyingine zozote, bali kundi la watu ambao wanamjua  vema Mungu wao, na wanaelewa kabisa wanachokwenda kukifanya ni nini, Ni watu ambao wameshaonja Baraka na neema zote za Bwana, hawa ndio haiwezekani kuwageuza upya wakatubu pale wanapoanguka. Biblia inasema wanachofanya ni  sawa na kumsulibisha Yesu mara ya pili.

> Sasa swali linakuja wanamsulibishaje mwana wa Mungu mara ya pili, na wanamfedhi kwa namna gani?

Tengeneza, picha mume amemfumania mke wake katika uzinzi. Sasa kutokana na yale maumivu ya kusalitiwa akataka kumfukuza, lakini Yule mwanamke akamlilia kwa kumwomba msamaha, akikiri kuwa hatarudia tena uovu ule, asamewapo. Basi Yule mwanamume akamsamehe, na kuachilia uchungu wote, maisha yakaendelea. Lakini baada ya kipindi kupita Yule muma akamfumania tena mke wake katika uzinzi, Unadhani kitendo kile kitanyanyua hisia gani kwa Yule mwanaume?

Bibla shaka ataona ni kama ametoneshwa majeraha ambayo yalishapona zamani kwa gharama kubwa alizoingia kumsamehe wakati ule. Ni sawa, anakumbushwa yale maumivu ya mwanzo. Ndivyo ilivyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, pale unapoacha wokovu ambao umeshaujua uzuri wake, kisha ukarudia yale yale maisha ya kale, ni sawa na kumrudishia Kristo maumivu aliyoyapata pale msalabani siku ile alipokusamehe dhambi zako. Unamsulibisha mara ya pili. Unampa mateso ambayo tayari alishayamaliza, unakuwa huna tofauti na wale waliompiga pale masalabani.

>Lakini hapo anaposema unamfedhehi kwa dhahiri. Anamaana ya unamzalilisha kwa wazi (yaani hadharani).

Chukua tena mfano; Mtu ameingia gharama ya kukupikia chakula kizuri cha heshima, akitarajia kuwa  utakapokula utakifurahia na kukipenda. Lakini ulipopewa kukila ulionyesha kukipenda pale mwanzoni, mara ghafla ukakichukia na kukitema mbele yake, na baadaye ukakimwaga, na baada ya hapo ukaenda kununua chakula chako kingine,ukala tena mbele yake. Jiulize Yule mpishi wako atajisikiaje?

Ataona umemfedhi, umemzalilisha, kama vile kazi aliyoifanya kwako ni bure, . Ndivyo Bwana, anavyoona, wale wanaorudi nyuma. Wanamdhalilisha, kuifanya kama vile kazi ya msalaba, inamapungufu fulani, ni ujinga tu uliofanyika pale, Roho Mtakatifu ni uongo, nguvu za Mungu ni dhaifu. Na ndio maana umeamua kugeukia mambo ya kidunia  uliyokuwa umeyaacha zamani.

Hivyo hatua kama hii, ni mbaya sana. Vifungu hivi ni kutufundisha zipo hatari nyingi kwa mkristo anayerudi nyuma kwa makusudi. Kamwe usiruhusu jambo hilo maisha mwako.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

FUVU LA KICHWA.

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

MJUE SANA YESU KRISTO.

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments