Swali: Pepo za Mbisho ni nini?
Jibu: Turejee kuanzia mstari wa 23.
Mathayo 14:23 “Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; MAANA UPEPO ULIKUWA WA MBISHO.
25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu”.
Maana ya neno “Mbisho” ni “Ukinzani”. Hivyo hapo aliposema “Upepo ulikuwa wa Mbisho”, maana yake upepo ulikuwa ni wa ukinzani, (yaani ulikuwa unavuma kinyume na uelekeo waliokuwa wanauendea).
Utasoma tena aina ya upepo huu ikitajwa katika Matendo 27:4,
Matendo 27:4 ”Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana PEPO ZILIKUWA ZA MBISHO”.
Safari yoyote ya majini, ikikutana na pepo za mbisho, safari hiyo inakuwa ni ngumu sana.. Kwasababu upepo utakuwa unavuma kinyume na ile merikebu na hivyo kuchelewesha safari au hata kuirudisha nyuma.
Lakini pepo za Mbisho zinafunua nini kiroho?
Pepo za mbisho kiroho ni kila aina ya matatizo, na shida na dhiki na vikwazo kutoka kwa yule adui vinavyokawisha au kurudisha nyuma safari yetu ya Imani hapa duniani.
Ndio maana utaona katika habari hiyo ya Mathayo 14:23-36, kabla wanafunzi wa Bwana YESU kufika nchi ya Wagerasi kwaaijli ya huduma ya kufundisha na kuponya wagonjwa na kuwafungua walioteswa na shetani, adui aliwatumia “Upepo huu wa mbisho”, lengo ni ili wasifanikiwe safari yao hiyo.
Lakini BWANA YESU alipoingia ndani ya chombo kile ule upepo ukakoma na misuko suko yake, kufunua kuwa zile zilikuwa ni hila za ibilisi.
Hivyo hata sisi tunapokutana na pepo za namna hii katika Imani, suluhisho ni kuzikemea kwa Imani na kwa jina la YESU, na zitatii.
Bwana akubariki.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.
About the author