Kama umeokoka kikweli kweli kwanini uchawi uwe na nguvu kwako??
Hesabu 23:22 “Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama NGUVU ZA NYATI.
23 Hakika HAPANA UCHAWI juu ya Yakobo, WALA HAPANA UGANGA juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!”
Umewahi kujiuliza kwanini Nguvu za Mungu zifananishwe an za NYATI kipindi anawatoa wana wa Israeli Misri na kuwapeleka nchi ya ahadi??..Je unajua tabisa za nyati ni zipi mpaka zifananishwe na za Mungu?
NYATI ni Mnyama jamii ya Ng’ombe, na anafanana sana na Ng’ombe… lakini ana nguvu nyingi kuliko Ng’ombe.. Lakini tabia za huyu mnyama ni kwamba HAKUBALI KUFUNGWA NA MTU na ANAWAPIGA WOTE WANAOJARIBU KUMSOGELEA.. Laiti angekubali kufungwa na mwanadamu basi angekuwa nyenzo moja bora sana ya kazi.. kwani ana nguvu kuliko Ng’ombe.
Kwa nguvu alizonazo huenda matrekta ya kulimia yangekosa soko, kama angekubali kufungwa NIRA kama Ng’ombe!..Lakini hakubali kufugika ingawa ni Ng’ombe, mwenye sifa zote za kufugika lakini hafungiki….Nguvu zake anazimalizia kutishia na kudhuru maadui zake na wote wanaomsogelea, wakati Ng’ombe ni mnyenyekevu na mwenye kukubali NIRA. .
Ayubu 39:9 “Je! Nyati atakubali kukutumikia? Au atakaa katika zizi lako?
10 Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani? Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako?
11 Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi? Au, utamwachia yeye kazi yako?
12 Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani. Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?”
Sasa tabia hiyo ya NYATI ya kukataa KUFUNGWA Nira, na BADALA YAKE KUWADHURU WANAOMSOGELEA KWA NGUVU ZAKE..ndiyo ilikuwa ndani ya WANA WA ISRAELI, walipokuwa wanasafiri jangwani.. Hakuna aliyewafunga tena Nira ya utumwa tena, na walikuwa wanawapiga maadui zao.
Pale ambapo Balaamu aliyekuwa mchawi (Yoshua 13:22) alipojaribu kuwalaani (yaani kuwafunga nira kichawi/kuwaloga), Ilishindaka kwasababu wanatembea na NGUVU ZA NYATI, ASIYEKUBALI NIRA!. Balaamu alipojaribu kuwafunga Mafundo kiroho ili wawe wanyonge mbele ya Balaki alishindwa, ule uchawi uligota.
Na Balaamu-mchawi alipoona kwamba mambo hayawezekaniki…Ndipo akasema, “HAKUNA UCHAWI WALA UGANGA JUU YA YAKOBO” Maana yake hakuna Nira ya kichawi wala ya kiganga kwa wana wa Israeli wanatembea kwa nguvu kama za NYATI…
Hesabu 23:22 “Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama NGUVU ZA NYATI.
23 Hakika HAPANA UCHAWI juu ya Yakobo, WALA HAPANA UGANGA juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!”
Je umeokoka na hizi nguvu zinatembea nawe?
Kama bado hujaokoka kikamilifu basi ni haki yako kuuogopa uchawi tena uugope sana!!. Lakini ukitaka usiuogope wala usiwe na nguvu juu yako suluhisho si kutafuta maji, au mafuta ya upako.. bali suluhisho ni wewe kuwa Israeli wa kiroho..Ukiwa Isreali wa kiroho uchawi unadunda, kwasababu utakuwa unatembea na NGUVU ZA NYATI ndani yako.
Na unafanyikaje Israeli wa kiroho?..Si kwa njia nyingine Zaidi ya kutubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Ikiwa utahitaji msaada wa kuongozwa namna ya kumpokea Bwana Yesu na kubatizwa basi waweza wasiliana nasi kwa namba zetu.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?
About the author