KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA.

KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA.

Jina la BWANA wetu YESU KRISTO lihimidiwe daima.

Neno la Mungu linasema..

Isaya 54:17 “KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA Kila na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana”.

Hapo anasema “kila silaha itakayofanyika haitafanikiwa” na si “kila shambulizi halitafanikiwa”.. Maana yake katika tu mwanzo wa maandalizi ya silaha, huo ndio hautafanikiwa!..

Kivipi?

Silaha za zamani zilikuwa ni Mikuki, Panga na Mishale na nyinginezo baadhi ambazo zote zilikuwa zinatengenzwa kwa vyuma na Wahunzi..(Sasa kufahamu mengi kuhusu Wahunzi na jinsi wanavyofua vyuma basi fungua hapa >>> Mhunzi ni nani? (Isaya 54:16) ).

Hivyo Wahunzi walikuwa wanayeyusha chuma kisha wanakitengeneza kwa umbile la silaha waitakayo kama ni panga, au kisu au mkuki.. Sasa hapa biblia inasema silaha yoyote inayotaka kutengenezwa na hawa wahunzi, haitafanikiwa..

Maana yake wahunzi wakiwa katika zile hatua za kuyeyusha chuma, basi hawafanikiwa kufikia hitimisho la kuikamilisha  ile silaha, maana yake shughuli yao itaishia katikati na hakuna silaha yoyote itakayozaliwa. (aidha wakiwa katika utengenezaji wataungua moto, au watapungukiwa na malighafi, au watapata hitilafu nyingine yoyote ambayo itawafanya wasilamize ile kazi).

Watabaki na chuma kisicho na umbile lolote la kisu, au sime, au panga au mkuki..

Isaya 54:16-17 “Tazama, nimemwumba MHUNZI avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu…kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa”

Vile vile na agano Mungu analoingia na watumishi wake ni agano la namna hiyo hiyo, maana yake hawataona hata dalili ya silaha juu ya maisha yao kwani Bwana ataziharibu kabla hazijakamilika…

Kama ni uchawi ndio silaha ya adui, basi wakati tu unapikwa huko kwenye vibuyu na miti, na makaburini na habarini au katika madhabahu za baali basi utaungua moto kabla haujakamilika (wala hutajua kama kuna mashambulizi yalikuwa yameandaliwa dhidi yako, hutaona hata hiyo dalili..mambo yanaharibika kabla hayakamilika)… baadaye sana ndio utakuja kusikia ushuhuda kwamba kuna njama zilipangwa juu yako na zikashindikana (kama Bwana ataruhusu ujue).

Kama magonjwa ndio silaha ya adui anayoisuka juu yako, akiwa katika kiwanda chake cha kukutengenezea hayo, Bwana atasimama kinyume chake na kuziharibu hizo hila, na hutaona chochote na wala kujua chochote kwani hata dalili haitaonekana.

Kama ni kuondolewa kazi ndio silaha ya adui, basi kabla hata hiyo mipango kukamilika, itafutwa na Bwana na kuharibiwa..(utakuja kujua tu baadaye kama Bwana ataruhusu ujue).

Na hiyo ndio sababu kwanini kuna umuhimu wa kumshukuru Mungu kila wakati kwani kuna vitu vingi sana Bwana anatuepusha navyo pasipo hata kuona dalili yake..

Kama ni visa ndio silaha ya adui ili upotezi hiki au kile Bwana alichokupa, basi kabla hivyo visa havijakamilika Bwana ataviharibu.. Hiyo ndio maana ya “kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa”.

Lakini hiyo ni kama wewe ni mtumishi wa Mungu (Maana yake unayempendeza Mungu na kuyafanya mapenzi yake)

Isaya 54:17 “SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA Kila na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana”

Lakini kama upo nje ya Kristo, basi fahamu kuwa kila silaha itakayofanyika juu yako itafanikiwa na itakudhuru.. Hivyo usiruhusu silaha yoyote ifanikiwe juu yako… Ni sharti iharibiwa ikiwa katika hatua zake za matengenezo, na wenye nguvu za kuweza kuharibu silaha hizo ni wale tu walio ndani ya imani.

Je umempokea Bwana YESU?.. Kama bado huu si wakati wa kupoteza muda, wala kungoja ngoja..ni wakati wa kujiokoa nafsi yako, wala si wakati wa kutazama nyuma, kama mke wa Lutu, bali ni wakati wa kupiga mbio na kuikimbia Sodoma..

Luka 17:32  “Mkumbukeni mkewe Lutu.

33  Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

TUZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA.

Mata ni nini (Mwanzo 27:3).

Kombeo ni nini? Teo ni nini katika biblia?

Fahamu ni nani aliye mwandishi wa kitabu cha Mathayo.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments