Leo hii kumekuwa na hofu nyingi katikati ya watu, juu ya historia na machimbuko ya familia zao. Wengine wameona maisha yao au tabia zao za sasa zimeathiriwa na chimbuko la familia zao, au koo zao, au mababu yao. Na hivyo hawajui wafanyeje.
Lakini ukweli ni kwamba hakuna hata mmoja wetu ambaye, chimbuko lake halijaathiriwa, Tukianzia na la Bwana wetu Yesu Kristo, na ndio maana biblia imeandikwa tukapewa, ili kutuonyesha sisi njia, ya kusimama na shindana na nguvu za Yule mwovu kwa ujasiri wote bila woga.
Kitabu cha Mathayo, kinaanza na kueleza ukoo wa Yesu. Kulikuwa na sababu ya kutangulizwa historia ya ukoo wake, ili Mungu kutufundisha sisi jambo. Watu wengi wakiangalia ule mtiririko, wanadhani Mungu anatuonyesha jinsi Yesu alivyotokea katika ukoo hodari, mashuhuri. Lakini Hapana. Ukweli ni kwamba hakukuwa na umuhimu wowote, kwa wengi walioorodheshwa katika ukoo wake.
Lakini nataka tuone, jinsi ukoo ule ulivyovurugwa, kiasi kwamba kama Mungu angetazama usafi basi, usingestahili hata kidogo kumleta mkombozi duniani. Katika ukoo wake hakukuwa tu na wema, lakini kulikuwa na “makahaba” kulikuwa na pia “wazinzi-waliokubuhi”, kulikuwa na “makafiri” . Kwamfano Yule Rahabu, alikuwa ni kahaba, tena kahaba kweli kweli. Tena Kulikuwa na Ruthu, mwanamke wa kimataifa, ambaye Mungu aliwakataza kwa nguvu sana, wayahudi wasitwae wanawake wa kimataifa kuwaoa, mbegu takatifu zisichangamane na mbegu nyingine (Ezra 9:2) ni unajisi, lakini hapa ikawa tofauti, mwanamke wa kimataifa akaingizwe kwenye ukoo. kama huyo haitoshi alikuwepo mzinzi Tamari, ambaye, yeye alifanya hila akalala na mkwe wake, kumzaa Peresi,..Jambo lisilofikirika kiakili, vilevile, alikuwepo Bersheba mke wa wizi, wa Mfalme Daudi, ambaye miongoni mwa wake halali wa Daudi hakuwepo, lakini alichaguliwa yeye, kuupitisha uzao wa Kristo, na wale wasafi wakaachwa.
Tusome..
Mathayo 1:1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
2 Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;
3 Yuda akamzaa Peresi na Zera KWA TAMARI; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;
4 Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;
5 Salmoni akamzaa Boazi KWA RAHABU; Boazi akamzaa Obedi KWA RUTHU; Obedi akamzaa Yese;
6 Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani KWA YULE MKE WA URIA ;
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;
9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;
10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;
11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.
12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;
13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;
14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;
15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;
16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.
17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vine.
Hivyo ukoo wa Bwana wetu Yesu Kristo, ulivurugwa-vurugwa, tunaweza kusema haukuwa msafi, kulinganisha na koo za wayahudi wengine. Lakini huyo ndiye aliyekuja kumpendeza Mungu kuliko wote, ijapokuwa alitokea katika chimbuko lililokorongoka, huyo ndiye aliyekuja kuwa mkombozi, huyo ndiye aliyekuja kuwafungua watu na kukata mizizi yote ya laana, na kuwa Baraka kwa ulimwengu.
Usiogope, yawezekana kweli, chimbuko lenu ni bovu, ni makahaba tu, ni walevi tu, mna magonjwa ya kurithi yanatembea, mnaudhaifu Fulani, maskini wa kupindukia, hamuoelewi, hamzai. Nataka nikuambie wacha kuhangaika kuufikiria ukoo wako. Kwasababu hata iweje hakuna aliyewahi kutokea mwenye chimbuko safi hapa duniani. Wewe mtazame Kristo tu, aliyemaliza yote pale msalabani. Amini tu kazi yake aliyoimaliza kwako.
Unapookoka, huna laana yoyote ndani yako, haijalishi ukoo mzima walizindika, haijalishi mna mizimu na mikoba ndani.. Hiyo ndio bye! Bye!, imeisha!. Haina nguvu ndani yako, wala usiipe kibali, mwamini Yesu aliyekukomboa.
Usiwe mtu wa kuzunguka huku na huko kuvunja laana za ukoo, utavunja ngapi? Ni mababu wangapi wamepita huko nyuma, itakupasa basi urudi sasa mpaka Adamu. Uvunje laana zote. Hivyo kua kiroho, mwamini Yesu aliyekukomboa. Matatizo ya kifamilia mliyonayo, wanayo hata wale watumishi wa Mungu, isipokuwa kwa namna tu nyingine. Lakini wao wamemwamini Kristo aliyewakomboa, ndio maana hawana laana yoyote. Lakini kaulizie huko kwao kukoje watakuambia. Ndugu ukiokoka, Ya kale yamepita tazama, yamekuwa mpya. Unachopaswa kufanya baada ya kuokoka tu , ni kuendelea kumjua zaidi Kristo ili uwe na amani,sio kuchimbua tena ya kale, jifunze kwa ukoo wa Yesu .
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini vizazi vya ukoo wa Yesu vinajipinga katika Mathayo na Luka.
About the author